Mpaka kufikia sasa hivi kampuni ya Facebook ina thamani ya dola bilioni 364, ambapo watu takribani bilioni 1.71 wanaingia katika mtandao huo kila mwezi.
Hii ndiyo stori nyuma ya mafanikio hayo makubwa ya Facebook, tokea kuanzishwa mwaka 2004 mpaka leo hii.
Facebook ilianzia katika bweni la chuo kikuu cha Harvad nchini marekani, mwaka 2003 kijana aliyefahamika kwa jina la Mark Zuckerberg ambaye alikuwa anasoma chuoni hapo alitengeneza programu aliyoipa jina la "Face mash". Ilikuwa ni programu ambayo watumiaji wake waliweza kutoa maoni ya picha zilizowekwa kama mtu ni mzuri au mbaya ambapo picha nyingi za watu zilizowekwa kwenye mtandao huo alizidukua kutoka kwenye mfumo wa udahili wa chuo ambao ulikuwa na picha za wanafunzi. ndani ya masaa manne mtandao huo uliweza kutembelea na zaidi ya watu 22,000, uongozi wa chuo uliamuru mtandao huo kuzimwa kutokana na usalama wa taarifa za watu zilizowekwa kwenye mtandao huo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MASSHELE BLOG SHARE POSTS SOMA ZAIDI HAPO CHINI KISHA CLICK PICHA ZILIZOPO JUU
Mark Zuckerberg akiwa bwenini
Zuckerberg alipewa adhabu na uongozi wa chuo lakini hakufukuzwa chuoni hapo. Mwezi wa pili mwaka 2004 jamaa alitengeneza mtandao mwingine alioupa jina la "TheFacebook".
Muonekano wa ukurasa wa kwanza wa facebook
Siku sita baada ya kuanzishwa kwa mtandao huo washkaji watatu ambao walikuwa mwaka wa mwisho chuoni hapo Cameron, Tyler pamoja na Divya Narendra walimshtaki Zuckerberg kwamba aliwaibia mawazo yao ya kutaka kutengeneza mtandao wa wanafunzi baada ya wao kumwambia washirikiane kutengeneza tovuti ya 'HarvardConnection.com' badala yake yeye aliachana nao na kutumia mawazo yao kutengeneza Facebook.
Cameron na Tyler
Jamaa walishinda kesi hiyo na kulipwa dola milioni 1.2. Ndani ya mwezi mmoja nusu ya wanafunzi wa chuo cha Harvad walikuwa ni watumiaji wa mtandao wa facebook. Ilipofika mwezi wa tatu 2004 facebook iliweza kukua zaidi hata mpaka kwenye vyuo vingine. Zuckerberg aliwaita baadhi ya rafiki zake kutoka Harvad, Dustin Moskovitz(kwenye picha kushoto) na wengine kama wasaidizi wake ili kuweza kukuza mtandao huo uwe wa biashara.
Zuckerberg akiwa na Dustin Moskovitz
Mpaka kufikia hatua hii Facebook ilikuwa bado inaendeshwa kwenye chumba cha Zuckerberg, ila jamaa aliacha masomo yake chuoni Harvard mwaka 2004 kama ilivyokuwa kwa Bill Gates.
Zuckerberg akiwa kwenye chumba chake Harvad
Mwezi wa sita 2004, Facebook ilihamishia ofisi zake Palo Alto, California, kwenye moja kati ya viofisi vidogo mjini humo. Kipindi hicho ofisi yao ilikuwa ni kama sehemu ya kusherekea.
Pombe zilikuwa ni kawaida ofisini hapo
Mark Zuckerberg aliweza kushinda ofisini na kipensi, pekupeku huku akiwa na kikombe cha bia.
Zuckerberg akiwa ofisini na kipensi huku akipata bia
Kiukweli jamaa walikuwa wanapenda sana bia cheki hii picha.
Hii ilikuwa si ofisi bali ni baa
Kuta za ofisi zote zilikuwa na michoro ya grafiksi.
Michoro ikiwa inaonekana ukutani mwa ofisi ya facebook
Kwa mara ya kwanza facebook walipata mwekezaji ambaye alikuwa ni mmoja kati ya watu walioanzisha PayPal, Peter Thiel (kushoto) ambaye aliwekeza dola 500,000.
Peter Thiel akiwa na Elon Musk waanzilishi wa PayPal
Facebook ilianza kukua kwa kasi nakuongeza maboresho mengi zaidi kwenye mtandao huo mwaka 2006 Facebook waliweka mfumo wa News Feed ambao unakuwa unaonesha watumiaji marafiki zao vitu wanavyofanya.
Mark Zuckerberg na kundi zima la facebook wakizindua Newsfeed
Facebook iliendelea kukua siku hadi siku pamoja na watumiaji wengi kuongezeka zaidi mwanzoni mwa mwaka 2010 facebook ilifikia watembeleaji trilioni moja kwa mwezi.
Facebook ilifikia watembeleaji 1,000,000,000,000 kwa mwaka 2010
Zuckerberg alifunga ndoa na mpenzi wake wa zamani Priscila Chan, ambaye walianza uhusiano wao tangu walipokuwa chuoni Harvad.
Zuckerberg akiwa na Priscila Chan
Facebook walinunua mtandao wa kushirikishana picha wa Instagram 2012 kwa dola bilioni 1 mtandao huo ambao unawatumiaji zaidi ya milioni 400.
Facebook waliununua mtandao wa instagram kwa dola bilioni 1
pamoja na mtandao wa kutumiana ujumbe wa WhatsApp ambapo facebook waliununua kwa dola bilioni 19 mwaka 2014. Mtandao huo kwa sasa ambao unawatumiaji zaidi ya bilioni 1 kwa mwezi.
Facebook waliununua mtandao wa kutumiana ujumbe WhatsApp kwa dola bilioni 19
Ili kukizi idadi kubwa ya wafanyakazi 2,800 facebook wameongeza ofisi zao mwaka huu wamefungua ofisi za jengo lao jipya ambalo limebuniwa na injinia Frank Gehry ambaye ni mzoefu.
Eneo la ofisi mpya za Facebook
Mwaka 2015 mwezi wa kumi na mbili Zuckerberg alitangaza kuchangia asilimia 99% ya utajiri wake wote katika foundation yake ambayo inahusika na kusaidia jamii maskini.
Zuckerberg na mkewe Chan
ASANTE MTU WANGU KWA KUTEMBELEA BLOG HII NAKUKARISHA KUSHARE AIDIA YOYOTE NAMI +255766605392
0 Comments