Bado stori za usajili Simba zikiendelea kutawala na majina makubwa kama yaEmmanuel Okwi kutoka Uganda na WalterBwalya kutoka timu ya Nkana yaZambia kuna tetesi za kukaribia kujiunga na Simba muda wowote wiki hii.
Leo June 15 2017 Simba imetangaza kumsajili mchezaji wa saba kwa msimu huu, Simba leo mbele ya makamu wa Rais wa club hiyo Geofrey Nyange Kaburuwameingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Ally Shomari anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa msimu huu na Simbawakiwemo pamoja na Aishi Manula,Shomari Kapombe na John Bocco, hata hivyo licha ya kuendelea kusajili Simbakuna tetesi kuwa imeachana na mshambuliaji wake Ibrahim Ajib kwa kushindwa kufikia dau la kusaini mkataba mpya.
0 Comments