Header Ads Widget

Responsive Advertisement

DALILI ZA HATARI WAKATI WA UJAUZITO





Wakati wa ujauzito, afya ya mtoto wako ni ya kwanza kuzingatia  ndo maana matatizo ya ujauzito yanaweza kuwa ya kuogopesha kwa sababu usipokuwa makini unaweza kupoteza ujauzito ama kujifungua mtoto mwenye matatizo

Kama una magonjwa sugu kama kisukari, kifafa au huzuniko-depression unatakiwa kuelewa jinsi gani magonjwa haya yanaweza kudhuru afya yako na mtoto au unatarajia madhara gani kutokana na magonjwa hayo na kujua kinagaubaga kuhusu matibabu yake na jinsi yanavyomwathiri mtoto. Ukijua haya unaweza kuzuia madhara kwa mtoto

Hata kama matatizo yanaweza kuwa makubwa sana katika kichwa chako, mtaalamu wa afya anaweza kufanya liwezekanalo kuhakikisha kwamba unakuwa na ujauzito wenye afya njema na unatakiwa ugndue umuhimu wao na ufanye maamuzi sahihi ya kuonana nao ili upate msaada unapohitajika

Baadhi ya dalili hatari wakati wa ujauzito zimeorozeshwa hapa chini, upatapo dalili hizi onana na mtaalamu wa afya haraka

  • Kutokwa na maji ya uzazi-kupasuka kwa chupa ya uzazi mapema zaidi katika ujauzito
    • Chupa ya uzazi kupasuka huwa si kitu rahisi na tatizo hili linapotokea linaweza kumaanisha maambukizi katika kuta za chupa ya uzazi au mgandamizo kwenye tumbo uliosababishwa na kupigwa, kuangukia tumbo au kitu chochote kinachoweza kuleta mgandamizo wa nguvu tumboni
    • Chupa ya uzazi ikipasuka inakuweka hatarini kupata maambukizi kwenye kizazi na mtoto hivyo huweza kusababisha ujauzito kutoka

  • Kutokwa na damu kipindi cha ujauzito
    • Kutokwa na damu kipindi cha ujauzito huweza kumaanisha jambo la hatari au lisilo la hatari linaendelea mwilini. Kipindi cha miezi mitatu ya kwanzaambapo kondo la nyuma huwa linatengenezwa kwa kuvamia ukuta wa uzazi huweza kusababisha mwanamke kuona damu lakini huwa sio nyingi sana wala hakuna maumivu ya tumbo. Endapo damu inatoka sana onana namtaalamu wa afya upate kufanyiwa uchunguzi
    • Mambo mengine yanayoweza kusababisha damu katika ujauzito niSaratani ya shingo ya kizazi,saratani ya mfuko wa kizazi,
  • Maumivu ya kichwa kutapika kupita kiasi au shinikizo la damu la juu, maumivu ya tumbo na kutoona vizuri(kuona vitu vimefifia)
    • Dalili hizo zinaweza kumaanisha mama amepata shinikizo la damu linaloelekea kuwa kifafa cha mimba au kitaalamupreeclampsiaau,shinikizo la damu la damu sugu na kifafa cha mimba/eclampsia.
    • Maumivu ya tumbo ya kubana na upande mmoja wa nyonga na maumivu kwenye bega la kizunguzungu kichefuchefu na kutapika miezi  mitatu ya kwanza ya ujauzito, mara nyingi hutokea kama mimba imetungwa nnje ya mfuko wa kizazi. Mama na awahi hospitali kwa uchunguzi zaidi ili kuondokana na matatizo ya kuvilia damu kwenye tumbo mara baada ya ujauzito huo kupasuka na hivyo kupoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi

  • Kutokwa na uchafu unaonuka ukeni
    • Saratani yashingo ya kizaziinaweza kuleta dalili kama hii, maambukizi pia katika uke au mfuko wa kizazi huweza kusababisha pia. Mama ni vema kwenda kituo cha afya kwenda kupima afya yake

  • Maumivu makali ya tumbo ya kubana mapema zaidi katika miezi mitatu ya pili ya ujauzito
    • Maumivu ya tumbo kabla ya wiki 37 za ujauzito humaanisha uchungu kabla ya muda kufika au preterm labor tatizo hili linaweza kusbabishwa na mabmo mengi kama vile magonjwa sugu ya mama (kisukari kisichodhibitiwa), maambukizi ya ukke au kizazi au wakati mwingine kama mama anamapacha tumboni. Ni vema kujua kuhusu afya yako kwa kumtafuta mtaalamu wa afya akufanyie vipimo na matibabu kama yatahitajika
  • Mtoto kupunguza kucheza au kutocheza tumboni kuanzia kipindi cha miezi 
    • ​Kuanzia wiki ya ishirini ya ujauzito mara nyingi mtoto huanza kucheza tumboni kwa mama, mtoto kucheza huonyesh mtoto yupo hai na anakua vyema. Mma aanatakiwa kujua namna mtoto wake anavyocheza ili akigundua mtoto amepunguza kucheza basi aonane na mtaalamu wa afya. Mtoto kutocheza au kupunguza kucheza huweza kumaanisha mtoto amefia tumboni ama mimba ilishatoka