DHANA YA TAFSIRI
Kwa mujibu wa Mwansoko na wenzake (2006) wanaeleza kuwa tafsiri ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine. Woa wanatilia mkazo katika zoezi la uhawilishaji na kinachohawilishwa ni mawazo katika maandishi.
Pia Catford (1965) anaeleza kuwa, kutafsiri ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha mmoja yaani lugha chanzi na kuweka badala yake mawazo yanayolingana kutoka katika lugha nyingine yaani lugha lengwa. Hapa msisitizo upo katika matini zilizoandikwa na kuzingatia zaidi ujumbe au wazo lililopo katika matini chanzi lijitokeze vile vile katika matini lengwa. Mawazo haya hayawezi kuwa sawa kabisa na ya matini chanzi bali ni mawazo yanayolingana toka matini chanzi na matini lengwa, hii ni kutokana na sababu tofauti kama vile utamaduni, historia, kiisimu na mazingira.
Naye Newmark (1982) anaeleza kuwa tafsiri ni mchakato wa uhawilishaji wa maneno kutoka matini chanzi kwenda matini lengwa.
Pia Nida na Taber (1969) wanaeleza kuwa tafsiri hujumuisha kuzalisha upya ujumbe wa lugha chanzi kwa kutumia visawe vya asili vya lugha lengwa vinavyo karibiana zaidi na lugha chanzi kimaana na kimtindo. Wao wanatilia mkazo uzalishaji upya wa kwa kutumia visawe asili vinavyokaribiana na matini chanzi kimaana na kimtindo. Kutokana na maana hizi tunaweza kusema kuwa tafsiri hufanywa katika ujumbe uliopo katika maandishi, ni jaribio la kiuhawilishaji na wazo linalatafsiriwa huwa na visawe vinavyokaribiana na sio sawa kutokana na tofauti za kiisimu, kihistoria, kiutamaduni na mazingira.
Kwa ujumla tunaweza kusema
Tafsiri ni taaluma inayohusika na uhaulishaji wa mawazo kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa kwa maandishi bila ya kupoteza , kupotosha na kubadili maaana .mawazo yanayoshugulikiwa katika taaluma ya tafsiri sharti yawe kwenye maandishi na yalingane kati ya lugha lugha asilia na lugha lengwa.
AINA ZA TAFSIRI
Tafsiri ya neno kwa neno , Hii ni tafsiri amboyo mofimu na maneno mengine hufasiriwa yakawa pwekepweke kwa kuzingatia maana zake za msingi bila kujali muktadha. Mpangilio wa mofimu na lugha chanzi hubaki vilivile , maneno yanayofungamana na utamaduni hufasiliwa kisisisi .matini ya tafsiri (matini lengwa) huwandikwa chini ya matini ya lugha chanzi
Mfano (1) Kiswahili : a – li – lala – hadi –asubuhi
Kiingereza : she /past /sleep/ until / morning
(ii) kiwahili : a -likwenda / nyumbani / kwke
Kiingereza : he / past / until /at /house /his.
Ø Ubora wa tafsiri neno kwa neno
Tafsiri ya aina hii humsaidia kumsaidia kuelewa jinsi lugha inavyofanya kazi katika kuanisha muundo
Ø Udhaifu wa tafsiri ya moja kwa moja
Upungufu wa tafsiri ya neno kwa neno ni kwamba mara nyingi haitoi kwa uangavu maana inayokusudiwa kwa sababu nahau na misemo inayohusika na utamaduni hufasiliwa kisisisi.
sababu nahau na misemo inayohusika na utamaduni hufasiliwa kisisisi.
Tafsiri sisisi
Kwenye aina hii ya tafsiri maneno hufasiliwa yakiwa pwekepweke kwa kuzingatia maana zake za msingi katika lugha chanzi bila kujali sana muktadha . lakini kufuatana na mfumo wa kisarufi ,hususani sintaksia ya lugha lengwa
Mfano kiingereza :He was taken a centrel police station
kiswahili : Alipelekwa kwenye kituo cha kati cha police ( badala ya kituo
kikuu cha police)
kiingereza :Dear listener , lend me your ears
kiswahili : Wasikilizaji wapendwa , niazimeni masikio yenu (badala ya naomba
mnisikilize.
Mfano Kiingeza : Two heads are better than one
Kiswahili : Mbili vichwa ni bora kuliko moja .(badala yake vichwa viwili ni bora
kuliko kichwa kimoja
Kizaramo : Zege dimlemelwe fisi ,mbwa domgela muhe.
Kiswahili : Mfupa uliomshinda fisi mbwa utampa pumu
Ø Ubora wa tafsiri sisisi :
Tafsiri hii husaidia sana mfasiri kuwa hakuna maaana ya kudumu ya maneno , bali maana halisi .Kutokana na matumizi yake katika muktadha maalumu aidha aina hii ya tafsiri hutumika sana katika tafsiri ya vichekesho kwani huibua ukinzani wa ajabu katika tungo .(Mfano; My name is Dr Livingstone I come from Johanesberg
Ø Upungufu wa tafsiri sisisi : Tafsiri sisisi agharabu hutoa tafsiri potofu na kwa hiyo huwa na uwezekano wa kuleta utata na hasara katika mawasiliano
Tafsiri ya kisemantiki/maana/uwazi/(semantic trasilation) hii ni aina ya tafsiri ambayo mfasiri huegemea zaidi kwenye kugha chanzi. Katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hufasiri kila neno katika sentensi jinsi ilivyo ila kwa kufuata sarufi hususani vipengele vya kisemantiki na kistakisia ya lugha chanzi.Katika aina hii ya tafsiri masahihisho au ya neno au jambo lolote unalodhani limekosewa haliruhusiwi isipokuwa uweza kuweka haya marekebisho hayo au ufafanuzi katika tanbihi. (mujibu wa( Catford na Nida 1965)
Mfano : Kizaramo : kihanga cha mkulu kilava nongo ya ugimbi.
Kiswahili : uso wa mkubwa umetoa mtungi wa pombe
Kizaramo :ngwengwe hadisolo jake
Kiswahili : dume la njani huwa na mamlaka zaidi katika eneo lake
Ø Ubora wa tafsiri :
Ubora wa tafsiri ni kuwa na uwezo mkubwa wa kuendeleza lugha legwa kwa kuingiza miundo na misemo toka lugha asilia .
Ø Udhaifu wa tafsiri :
tafsiri hii haitilii maanani nahau , misemo maalumu inayohusiana na utamaduni na lugha inayolengwa katika tafsiri . Mfano (Assaina married Mtillah. –kiwahili :Assaina alimuoa Mtillah) badala Asha kuolewa na Moses kwani katika Kiswahili mwanamke huwa anaolewa na mwanaume ndiye anaoa hii huweza kuleta utata katika lugha ya kiwahili kwa mwanamke ndiye kuoa na mwanaume kuolewa.
Tafsiri ya kimawasiliano ,
hii ni aina ya tafsiri ambayo huzingatia hadhira ya matini ya lugha lengwa kwa kumjali sana msomaji wa matini hiyo . hii ni tafsiri huru kwa sababu mfasiri anaweza kuongeza au kupunguza maneno ya matini ya lugha asilia wakati wa kufasili ili mradi ujumbe uwafikie kwa namna inayotakiwa na bila kupoteza wazo la matini ya lugha asilia, mfasiri ana uhuru wa kutafuta maneno au mafungu ya maneno yanayolingana na nahau,misemo ,methali , utamaduni na mazingira ya lugha lengwa
Ø Ubora wa tafsiri mawasiliano
Ubora wa tafsiri hii ya kimawasiliano ni kwamba hufuata kanuni taratibu na sheria za lugha lengwa na kuzingatia mweelekeo wake wa kiutamadudi ,kiistoria ,kimazingira na kijamii kwa hadhira lengwa
Mfano
Kiingereza : Veronika married chris
Kiswahili :chris alimuoa veronica
Ø Udhaifu wa tafsiri mawasiliano
Kutokuwa na uwezo wa kuendeleza ,kuingiza miundo au misemo kutoka lugha asilia kwenda katika lugha lengwa. Hali hii inatokana na ukweli kuwa tafsiri hii haizingatii miundo ,misemo , na msamiati wa lugha asilia wakati wa kufasiri bali huzingatia wazo la jumla la kiutamaduni kwa lugha lengwa
Udhaifu mwingine katika tafsiri ya kimawasiliano hujitokeza pale mfasiri anapoegea sana kwenye mawzo , historia ,utamaduni , mazingira na itikadi ya lugha lengwa . kwa mfano katika mwaka 2002 vyombo vya habari vilisikika vikitangaza
Mfano kiingereza : His excellency president saddam Hussein (vyombo vya habari vya
Iraq mwaka 2002)
Kiswahili :Gaidi saddam Hussein ( vyombo vya habari vya marekani mwaka 2002
Kutokuwa na uwezo wa kuendeleza ,kuingiza miundo au misemo kutoka lugha asilia kwenda katika lugha lengwa. Hali hii inatokana na ukweli kuwa tafsiri hii haizingatii miundo ,misemo , na msamiati wa lugha asilia wakati wa kufasiri bali huzingatia wazo la jumla la kiutamaduni kwa lugha lengwa
Udhaifu mwingine katika tafsiri ya kimawasiliano hujitokeza pale mfasiri anapoegea sana kwenye mawzo , historia ,utamaduni , mazingira na itikadi ya lugha lengwa . kwa mfano katika mwaka 2002 vyombo vya habari vilisikika vikitangaza
Mfano kiingereza : His excellency president saddam Hussein (vyombo vya habari vya
Iraq mwaka 2002)
Kiswahili :Gaidi saddam Hussein ( vyombo vya habari vya marekani mwaka 2002)
MAREJEREO
Catford J.C. (1965) A Linguistic theory of Translation: OUP London.
Mwansoko, H.J.M. na wenzake (2006) Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu: TUKI
Dar es Salaam.
Newmark, P. (1988) A Textbook of Translaton. : Prentice Hall London.
Nida, A. E. na Charles, R. T. (1969)The Theory and Practice of Translation. The United
Bible Societies: Netherlands.
Wanjala S. F (2011) Misingi ya ukalimani na tafsiri; Serengeti Education publisher (T)
L.T.D. Mwanza
