Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TATIZO LA KUKOSA USINGIZI (INSOMNIA)




Insomnia ni tatizo endelevu  linalosababisha mtu kushindwa kuanza kusinzia, kutodumu kwenye usingizi ama vyote viwili licha ya kupata fursa ya kulala ipasavyo.  Kwa kukosa usingizi, mtu huyu kwa kawaida huamka hajihisi kuwa mpya , hali hii inasababisha kupunguza uwezo wa kufanya kazi wakati wa mchana.kukosa usingizi hakumalizi nguvu tu na hali yako, bali hudhuru afya na ubora wa maisha.

Usingizi kiasi gani unatosha hutegemea mtu moja na mwingine,mara nyingi watu wazima huhitaji masaa 7 hadi nane ya kulala.

Watu wengi pia walishawahi au watapata tatizo la kukosa usingizi kipindi Fulani katika maisha yao lakini huwa si endelevu lakini baadhi wanaweza kupata tatizo hili na kuwa endelevu. Kukosa usingizi kupo kwa aina mbili yaani aina ya kwanza na aina ya pili amabayo husababishwa na madawa au ugonjwa mwilini.
Huhitaji kutolala usiku, mabadiliko ya mambo Fulani katika maisha yako yanaweza kukusaidia kupata usigizi.

Dalili
Dalili za kukosa usingizi huweza kuwa

  • Kushindwa kusinzia usiku
  • Kuamka wakati wa usiku
  • Kuamka mapema sana
  • Kutohisi umepumzika vema baada ya kuamka
  • Kuchoka wakati wa mchana au kukosa usingizi
  • Kuwa mkali, msongo wa mawazo au wasiwasi
  • Kukokuwa makini, kutojikita kwenye jambo moja au kutokumbuka
  • Kuongezeka kwa makosa au ajali
  • Maumivu ya kinchwa ya mgandamizo
  • Usumbufu katika matumbo na tumbo
  • Kuwa na hofu kuhusu kulala

Mtu mwenye tatizo la kukosa usingizi huchukua dakika 30 au zaidi ili kupata usingizi na hulala masaa sita au pungufu na hili hutokea mara 3 au zaidi kwa wiki moja au mara kwa mara usiku kwa mwezi au zaidi.

Wakati gani wa kuonana nadaktari?

Kukosa usingizi husababisha kupungua kwa ufanisi wakati wa mchana, unatakiwa umwone daktari ili kufahamu nini kinachosababisha na upate matibabu sahihi. Kama daktari ataona kwamba unatatizo sugu la usingizi atakupeleka kwa wataalamu wa usingizi kwa vipimo zaidi.

Visababishi

Visababishi vikuu ni;

Msongo wa mawazo-kuhusu shule, kazi, afya au familia huweza kusababisha akili yako ikafanya kazi usiku na kusababisha kushindwa kulala. Kipindi kigumu katika maisha kama kifo ugonjwa au kupoteza mpendwa, kuachika, kupoteza kazi huweza pelekea kukosa usingizi.

Wasiwasi- kupata wasiwasi kila siku husababisha tatizo la kukosa usingizi.

Msongo wa mawazo- unaweza kulala kupita kiasi au kukosa usingizi kama una msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo hutokea pamoja na matatizo mengine ya kiakili.

Hali ya kiafya- kama una maumivu sugu, upumuaji wa shida,au unakojoa mara kwa mara unaweza kupata tatizo la kukosa usingizi. Matatizo ya kiafya yanayoambatana na tatizo la kukosa usingizi ni maumivu ya michomo katika maungio, saratani, kufeli kwa moyo,ugonjwa kwenye mapafu, ugonjwa wa kucheua-GERD, kufanya kazi sana kwa tezi ya thyroid,kiharusi,ugonjwa wa  parkinson’s na alzheimer’s.

Kubadili mazingira au ratiba za kazi- kusafiri au kufanya kazi join au kuwa na shifti za kazi mapema huweza kubadili tabia ya mzunguko wa mwili na kusababisha kukosa usingiz. Tabia ya mwili huwa kama saa ya ndani ya mwili ambayo huongoza kila kitu kama mzunguko wa kulala na kuamkana michakato mbalimbali kwenye chembe hai mwilini na ujoto.

Kukosa ratiba ya kulala- kukosa ratiba ya kulala kama kutokuwa  na mda maalumu wa kulala, kazi za kuamsha mwili kabla ya kulala, mazingira yasiyo rafiki kwa ajili ya kulala, kutumia kitanda kwa kazi nyingine isipokuwa kulala ama kufanyia tendo la ndoa.

Madawa- madawa mbalimbali yanaweza kusababisha hali ya kukosa usingizi kama vile madawa ya kupambana na sononeko, madawa ya moyo na shinikizo la damu, madawa ya aleji, viamsha mwili kama Ritalin na corticosteroid. Madawa mengi ya dukani kama madawa ya maumivu, mabawa ya kuzibua pua na kupunguza uzito na matumizi.

Kahawa, nicotini na pombe- kahawa chai, cola na vinywaji vyenye virutubisho vya kahawa hujulikana kuwa ni viamsha mwili. Kunywa kahawa mchana au usiku huzuia mtu kupata usingizi usiku. Nicotine iliyo kwenye tumbaku na sigara huwa ni kiamsha mwili kingine kinachosababisha kukosa usingizi. Pombe hulegeza mwili na huweza kusababisha kusinzia lakini huzuia kufikia kilele cha usingizi na kwa kawaida husababisha kuamka wakati wa usiku.

Kula sana wakati wa jioni-kula chakula kidogo ni sawa, lakini kula kupita kiasi wakati wa jioni au usiku huwea kukusababisha hisia za kutohisi vema kama ukilala chini na kusababisha kushindwa kusinzia.watu wengi pia hupata kiungulia, kubeua, ambavyo humkosesha usingizi.


Kukosa usingizi na uzee
Jinsi mtu anavyozeeka huanza kupata mambo haya;

Kubadilika kwa tabia ya kulala. Usingizi hupungua jinsi mtu anavyozeeka na huweza kuamshwa na vitu vidogo kama makelele ama kubadilika kwa mazingira. Pia jinsi mtu anavyozeeka huchoka mapema na kulala jioni na pia huamka mapema. Lakini watu wazee wanatakiwa kupata mda sawa wa kulala kama watu wengine.

Kubadilika kwa kazi- kutojihusisha sana kwenye mambo ya kijamii na mazoezi. Kukosa kujihusisha kwenye mambo ya kijamii ama mazoezi hufanya kutopeza uwezo wa kupata usingizi usiku, pia watu hawa wanaweza kulala mchana ambapo huweza kusababisha wakakosa usingizi wakati wa usiku.

Mabadiliko ya kiafya-maumivu sugu kama yanayoletwa na hali kama michomo kwenye maungio au maumivu ya mgongo pamoja na sononeko, wasiwasi na msongo wa mawazo huchangia kutopata usingizi kwa wazee. Wazee wakiume pia huvimba tezi dume ambapo huchangia kukojoa mara kwa mara na hivyo kuamka sana usiku.

Madawa mengi- mzee huwa kwenye hatari  ya kutumia dawa nyingi kuliko vijana ambapo huongeza hatari ya kutopata usingizi kutokana na madawa.

Vihatarishi
Karibia kila mtu ameshawahi kupata tatizo la kutopata usingizi wakati wa usiku, vihatarishi vinavyoongeza hatari ya kutopata usingizi ni kama vile.
  • Kuwa mwanamke- kuwa mwanamke ni kihatarishi cha kutopata usingizi wakati wa usiku. Mabadiliko ya homoni mwilini wakati wa hedhi na wakati wa kukoma hedhi huchangia kwa wanawake. Wakati wa koma hedhi, kutokwa jasho hudhuru kupata usingizi. Pia mwanamke akiwa mjamzito kutopata usingizi hutokea sana.
  • Kuwa na umri zaidi ya miaka 60
  • Kuwa na matatizo ya kiakili
  • Kama sononeko, wasiwasi,
  • Kuwa na msongo wa mawazo mkali.
  • Kufanya kazi usiku wa kuwa na shifti kazini
  • Kusafiri umbali mrefu.

Madhara
Kulala ni jambo la umuhimu sana kwa binadamu ka vilivyo chakula na mazoezi. Haijalishi sababu inayosababisha kukosa usingizi, kukosa usingizi hudhuru hali ya kimwili, kisaikolojia. Watu wanaokosa usingizi huweza kupata mambo yafuatayo.

  • Ufanisi mdogo kazini na shuleni
  • Kupungua uwezo wa kukabiliana na mambo wakati wa kuendesha gari- kuongezeka wka ajali
  • Matatizo ya kiakili kama sononeko na wasiwasi
  • Kuwa na uzito mkubwa ama kitambi
  • Kuwa mkali
  • Kuwa na magonjwa ya mda mrefu yasiyo ya kuambukizwa kama shinikizo la damu la juu, magonjwa ya  moyo na kisukari
  • Ulevi
 Kwa vipimo na matibabu tutafute kwenye namba zetu zilizo Kwenye app yetu ama wasiliana na daktari wako popote pale ulipo kwa uchunguzi na matibabu