Katika taarifa waliyotuma katika mitandao yao ya kijamii waliandika yafuatayo
TANZIA
Uongozi wa Azam Media Limited umethibitisha vifo vya wafanyakazi wake watano wakiwa ni miongoni mwa watu saba waliofariki kwenye ajali ya gari iliyotokea kati ya Shelui na Igunga. Wawili wapo mahututi, mmoja hali yake si mbaya.
Ajali hiyo imetokea wakiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya kwenda kuonesha shughuli ya TANAPA ambapo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Rais John Magufuli
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi Ameen.
#WapumzikekwaAmani #AzamtvApp #AzamUTV #AzamTWO #UFMRadio

0 Comments