Kicheko ni kwa wawekezaji wa benki ya KCB, wakati wa Acacia, NMG na EABL watalala na maumivu.- Maumivu hayo yanatokana na thamani ya hisa za kampuni hizo kushuka kwa viwango tofauti.
- Benki ya CRDB yaongoza kwa kuuza hisa nyingi za asilimia 99.05.
Dar es Salaam. Wawekezaji wa benki ya KCB katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) wana kila sababu ya kutabasamu baada ya thamani ya hisa za benki hiyo kupaa na kuwafanya waweke kibindoni Sh10 kwa kila hisa moja kutoka kiwango cha jana Julai 2, 2019.
Ripoti ya soko ya siku ya DSE ya Julai 3 inaonyesha kuwa hadi soko linafungwa thamani ya hisa moja ya KCB ilikuwa ni Sh870 kutoka Sh860 iliyorekodiwa jana.
Hata wakati wawekezaji wa KCB wakinehemeka leo, wenzao wa kampuni ya habari ya NMG watalala na maumivu baada ya thamani ya hisa za kampuni hiyo kushuka kutoka Sh1,100 kwa hisa moja iliyorekodiwa jana wakati soko linafungwa hadi Sh1,080 leo hii jioni.
Kampuni zingine ambazo zimefanya vibaya leo sokoni ni pamoja na Acacia ambayo thamani ya hisa zake imeshuka kwa asilimia 0.98 na kampuni ya bia ya Afrika Mashari-EABL (asilimia 0.45).
Benki ya CRDB ndiyo kampuni iliyoongoza kwa kuuza kiwango kikubwa cha hisa za asilimia 99.05 ya hisa zote zilizouzwa sokoni leo na kufuatiwa kwa mbali na kampuni ya uwekezaji ya NICO huku zingine zikibaki katika viwango vilivyokuwepo jana zikiwemo Vodacom na TICL
.
.
0 Comments