Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Fahamu chanjo zinavyotengenezwa



  • Ili chanjo ianze kutumika inapita katika awamu tatu za majaribio.
  • Mpaka sasa chanjo sita zimehizinishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
  • Chanjo ya AstraZeneca ndiyo chanjo inayotumiwa na nchini nyingi za Afrika Mashariki.

Dar es Salaam. Chanjo zipo za ina nyingi na zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu huku mamilioni ya watu wakipatiwa chanjo hizo salama toka chanjo ya kwanza ilivyopatikana mwaka 1796 huko nchini Uingereza.
Kabla ya chanjo kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu hupitia hatua mbalimbali za majaribio ili kuithibitisha kama italeta  
Ifahamike kuwa katika hatua za majaribio huanza kupewa wanyama wakiwemo panya ili kupima ufanisi wake. Katika muda huo endapo chanjo italeta mwitikio mzuri wa kinga basi majaribio mengine huendelea.
Hatua inayofuata ni kuipelekwa kwa watu kwa awamu:
Awamu ya kwanza
Kwenye awamu hii chanjo hutolewa kwa idadi ndogo ya watu  kwa lengo la kutathamini usalama wake na kuangalia kama inafanya kazi kwa usahihi na kuamua kipimo sahihi kitakachotolewa.
Mara nyingi huhusiha vijana, watu wazima wenye afya njema waliojitolea.
Awamu ya pili
Katika awamu ya pili chanjo hutolewa kwa mamia ya watu kwa lengo la kufanyia majaribio ili kuangalia uwezo wake wa kujenga kinga.Sifa za washiriki katika awamu hii huchaguliwa watu kutoka katika makundi mbalimbali kwenye jamii ili kukidhi mahitaji ya kila kundi.
Kundi ambalo halikupata chanjo kwa kawaida hujumuishwa katika awamu kama kikundi cha kulinganisha ili kubaini ikiwa mabadiliko katika kikundi kilichochanjwa yametokana na chanjo au yametokea kwa bahati.
Awamu ya tatu
Kwenye awamu hii, maelfu ya watu hujitolea kuchanjwa ili kubaini ikiwa chanjo hiyo ni bora dhidi ya ugonjwa husika.
Majaribio katika sehemu hii huenda mbali zaidi ya mipaka ya jografia ambapo watu kutoka katika mataifa mbalimbali nao huusishwa katika majaribio hayo.
Wakati wote wa majaribio hayo, tathmini ya uhakiki wa ufanisi na usalama hufanyika kwa idhini ya ya sera za afya ya umma.
Chanjo lazima ithibitishwe kuwa salama na yenye ufanisi kwa idadi kubwa ya watu kabla ya kuidhinishwa na kuingizwa kwenye programu za kitaifa  za chanjo.  
Wakati chanjo inapoanza kutumika ni lazima ifuatiliwe kila wakati ili kuhakikisha inaendelea kuwa salama.Chanjo za Corona zilizoidhinishwa
Mpaka sasa Shirika la Afya ulimwenguni limerushu chanjo zipatazo 6 ambazo ni  AstraZeneca/Oxford , Johnson and Johnson, Moderna, Pfizer/BionTech, Sinopharm na  Sinovac.
Huku mataifa ya Afrika Mashariki ambayo ni Kenya, Uganda , Rwanda na Sudani ya Kusini, yamefanikiwa kuagiza chanjo ya AstraZeneca na kuwawapa wananchi wao.
Pia Tanzania tayari imejiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza upatikanaji wa chanjo wa COVAX kwa nchi za kipato cha chini kama ilivyo kwa nchi zingine za Afrika Mashariki  ili kuanza kuwapatia raia wake.

Post a Comment

0 Comments