1. Utangulizi.
Wataalamu mbalimbali wamefasili dhana ya sentensi kama ifuatavyo Kapinga (1983), anafasili sentensi kuwa ni kipashio kikubwa kuliko vipashio vya kiisimu na huwa na wazo kamili. Anaendelea kueleza kuwa sentensi ni sehemu ya sarufi ambayo agharabu hujisimamia kimaana, mala nyingi sentensi huweza kuwa na maana anbazo huweza kuwa ni taarifa, ombi, mashariti, au hata amri.
Richard et all (1985), anasema sentensi ni dhana asilia ya lugha ambayo
hufafanuliwa kudhihirisha sehemu ya sarufi yenye neno moja au zaidi
inayosimamia wazo kamili nae Radford (1997), anasema sentensi ni sehemu
ya sarufi ambayo hujisimamia kisintaksia na ambayo huwa na kiima na
kiarifu ambacho kina kitenzi kimoja au zaidi. Kwaujumla sentensi ni
tungo yenye muundo wa kiima na kiarifu na vilevile husimamia wazo kuu.
Sentensi huweza kuainishwa kwa mkabala wa kisemantiki (mapokeo) cha
maana ambapo kuna sentensi swali, sentensi maelezo, sentensi mshangao na
sentensi shurtia.
Vilevile sentensi huainishwa kwa mkabala wa kisasa (kimuundo) ambapo
kuna sentensi sahili, sentensi changamano, na sentensi ambatano.
Sentensi ya Kiswahili huwa na muundo anuai kama inavyo fafanuliwa hapa
Sentensi huwa muundo wa kiima. TUKI (2004) wanaeleza kiima kuwa ni neno
au kifungu cha maneno katika sentensi ambacho hutangulia kitennzi. Hivyo
muundo wa kiima katika sentensi ni sehemu ya sentensi ambayo
inatawaliwa na nomino, vilevile kinaweza kushirikisha kikundi kivumishi
au kishazi tegemezi, Mfano
Matunda matamu huvutia
K
Wanafunzi waliokuwa wametoka shuleni wameathibiwa
K
Muundo wa kiarifu. Kiaifu TUKI (2004), wanaeleza kuwa kiarifu ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi, shamirisho na shagizo.hivyo muundo wa kiarifu katika sentensi ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi ambayo hushirikisha kikundi kielezi au kikundi kivumishi, vilevile kinaweza kuwa na nomino kama shamilisho.
Mfano Mvua inarutubisha vitu vyote
A
Dunia huzunguka jua
A nzi kinaweza kuwa
Miundo ya Shamilisho ni miundo katika sentensi ambayo mtendwa au mtendewa katika sentensi ni sehemu ya sentensi inayowakilisha kitu kilichofanyiwa kitu. Aidha kirai kitenzi kinaweza kuwa na kirai nomino kama shamilisho.
Kwaujumla sentensi za Kiswahili huwa na dhima mahususi mahusiano yake ni tofauti na lugha ya ulaya vilevile sifa za lugha ya Kiswahili na lugha ya kibantu zinafanana, sifa hizo ni kama vile sentensi huwa na upatanishi wa kisarufi ambapo kiima hudhibiti virai vingine kwa kutumia viambishi vipatanishi. Mfano Mtu mrefu amekufa
Marejereo
Kapinga, M.C (1983), Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu:Dar es Salaam TUKI
TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu: Dar es saalama, TUKI
Massamba, D.P.B, Kihore, Y.M, na Hokororo J.I (1999), Sarufi Miundo ya Kiswahili Sarufi SAMIKISA Sekondari na Vyuo:Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili . Dar es Salaam

0 Comments