Vijana wenye hasira nchini Ghana katika eneo la Suame wamemfuata mbunge, huku wakimpigia makofi, kumtusi na kumrushia maji.
Kiongozi wa wengi, Osei Kyei Mensah-Bonsu alikuwa katika eneo hilo kuzungumza na watu juu ya mahitaji yao ikiwa ni pamoja na miundombinu duni.
Wiki iliyopita baadhi ya wakazi waliweka vizuizi barabarani kupinga hali ya barabara hizo.
Wakati kikundi cha mafundi wachanga kilipogundua kuwa Bw Mensah-Bonsu alikuwa katika eneo hilo walielekea moja kwa moja kwenye eneo la tukio na kuanza kusema kwa kelele ‘’ondoka, ondoka!’’.
Polisi walifika baadaye kutuliza ghasia.
Vijana hao walisema walimfukuza Bw Mensah-Bonsu, kwa sababu licha ya kuwawakilisha bungeni, hatimizi ahadi zake za kurekebisha barabara.
Bw Mensah-Bonsu alisema hana wasiwasi kuhusu tukio hilo kwa sababu vijana wangefanya vivyo hivyo kwa afisa yeyote wa serikali, na sio yeye peke yake

0 Comments