Wizara ya Afya kupitia kwa Mganga Mkuu wa Serikali Aifello Sichwale imethibitisha vifo vya Watu watatu ambao wamefariki kutokana na kuugua maradhi mapya ambayo bado hayajulikana jina lake Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
“Wizara ya Afya ilipokea taarifa toka kwa Mganga Mkuu Lindi kuwa Ruangwa kuna Ugonjwa usio wa kawaida kutoka Kituo cha Afya Mbekenyera, ambapo ndani ya siku 3 (tarehe 5 na 7 July 2022) walipokea Wagonjwa 2 wakiwa na dalili za homa, kuvuja damu (hususan puani), kichwa kuuma na mwili kuchoka sana”
“Wizara iliunda timu ya wataalam kutoka idara ya Magonjwa ya dharura na Majanga, Epidemiolojia, Mkemia Mkuu wa Serikali, NIMR, Chuo kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliungana na timu ya Mkoa ikihusisha Idara ya Mifungo”
“Hadi hadi kufikia tarehe 12 Julai kulikuwa na jumla ya Wagonjwa 13, kati yao, 3 wamefariki, wawili waliokuwa wametengwa katika kituo cha Afya Mbekenyera, wamepona, wengine 5 wamejitenga katika makazi yao ya muda kwenye kitongoji cha Naungo, Kata ya Nanjilinji Wilayani Kilwa”

0 Comments