Mchezaji wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi
TIMU
ya Taifa ya Argentina imeibuka mabingwa kombe la Dunia kwa mikwaju ya
Penati dhidi ya timu ya Taifa ya Ufaransa mara baada ya kutoka sare ya
2-2 kwa dakika 90 na 3-3 dakika 30 za nyongeza (extra time).
Argentina
ilianza kutangulia kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa kipindi cha kwanza
kupita kwa nyota wao Lionel Messi pamoja na Angle Di Maria na
kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele.
Kipindi
cha pili Ufaransa ilifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji wake,
mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwani walipata mabao mawili ya haraka
kupitia kwa kijana wao nyota Kylian Mbappe na kumfanya amzidi mpinzani
wake Lionel Messi kufikia mabao saba wakati mweznake akiwa na mabao sita
tu kwenye michuano hiyo.
Wakati huo huo Mchezaji wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ameibuka
kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya
kufanikiwa kuisaidia timu yake ya Taifa kutinga Fainali na kunyakua
kombe la michuano hiyo ambayo imepigwa nchini Qatar.
Messi
pia amefanikiwa kushika nafasi ya pili kwa wafungaji wa mabao kwenye
michuano hiyo akiwa na mabao saba huku Klyian Mbape akiibuka kuwa
mfungaji bora akiwa na mabao nane
.jpeg)

0 Comments