Header Ads Widget

Responsive Advertisement

DK KIKWETE AZUIWA UWANJA WA NDEGE

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amezuiwa kusafiri kwenda nje ya nchi katika Uwanjwa wa Ndege wa Kimataifa wa Kulius Nyerere jijini Dar es Salaaam baada ya mmoja wa wajumbe wake kutokuwa na viza ya kusafiria. Taarifa zilizoandikwa katika gazeti la Mtanzania zinaeleza kuwa Rais Kikwete alikuwa ameambatana na mkewe, Mama Salama Kikwete wakati tukio hilo likitokea jana jioni majira ya saa 10. Gazeti hilo liliendelea kueleza kuwa Rais Kikwete pamoja ya wajumbe wake walikuwa wasafiri kwenda Abudhabi kupitia Dubai jana jioni kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Emirates. Inaelezwa kwa kuwa ukaguzi wa ndege za kimataifa hufungwa saa moja kabla ya ndege kuanza safari ili taratibu nyingine zifanyike. Ndege ya Emirates ilikuwa iondoke saa 10:30 jioni lakini hadi zoezi la ukaguzi linafungwa mjumbe mmoja aliyekuwa na Rais Kikwete hakuwa amefanyiwa ukaguzi. Viza yake ilipofika saa kumi hakuweza kufanyika ukaguzi na ndege iliondoka. Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kuwa Rais Kikwete atasafiri leo kuelekea nchini Dubai baada ya kukamilisha taratibu zote

Post a Comment

0 Comments