Mashele kiswahili
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameathiri sana fasihi simulizi has a katika nyanja ya uwasilishwaji wake na uenezi wake.
Hivyo utaona kwamba ile fasihi simulizi asilia inakufa au kupoteza sifa, kutokana na watu wengi hupendelea sinema, muziki, nk ndiposa utakuta mababu kwa sasa wanakufa Bila kuridhisha hekima na maarifa kwa kizazi hiki kupitia fasihi simulizi.
Kutokana na maendeleo haya ya kisayansi na teknolojia, ile sifa ya kuonana ana kwa ana kati ya fanani na hadhira imekufa, hivyo hata ule ushiriki wa hadhira nao umepotea.
Katika uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi
1. Kichwani
zamani fanani msimuliaji analiweza kubadili namna ya usimuliaji kwa kuongeza vionjo na kulingana na hadhira Lakini katika karne hii ya 21 hakuna muda tena wa kusimuliana hadithi, ukibahatika kusikia hadithi basi utasikia runingani kama ITV, au katika redio 1 au DW je ule ushiriki wa awali na ile dhana ya kuchagua hadhira ipo?
2. Maandishi
3.Vinasa sauti
4.kanda za video
Kwa ujumla fasihi simulizi imepoteza ule uhalisia, haiwakutanishi tena ana kwa ana fanani na hadhira, haipokei tena mabadiliko ya papo kwa hapo, haichagui tena hadhira, mmomonyoko wa maadili, mwisho haiwezi kumfikia kila mtu kwa kuwa ni gharama.

0 Comments