Baada ya kutambulishwa rasmi, Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina amesema atapambana vilivyo kuhakikisha anafanya vema. Lakini Lwandamina raia wa Zambia, amekiri kuwa kweli ni jukumu gumu kwake kama changamoto. “Lakini nitapambana kufanya vizuri, najua ni changamoto mpya kwangu lakini nitafanya kila linalowezekana,” alisema. Lwandamina ambaye kwa mara ya kwanza alifanya mahojiano na masshele ameomba Wanayanga kumpa ushirikiano ili kufikia malengo yake. Awali aliwahi kuiambia masshele kwamba anapenda soka la kushambulia pia kukaba pamoja. Lakini akasisitiza suala la ushrikiano ni namba moja kwake.
0 Comments