FUNGA
MWANZO
HABARI
MAKALA
MAONI
KATUNI
HADITHI


Nyumbani Habari USAJILI YANGA NI VITA YA VIGOGO AFRIKA
HABARILATEST NEWS
USAJILI YANGA NI VITA YA VIGOGO AFRIKA
Na Bingwa - November 17, 2016 5242 0
Facebook Twitter

EZEKIEL TENDWA NA ZAINAB IDDY
NI wazi kwa sasa Yanga hawawezi kupambana na timu yoyote katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kwenye suala la fedha, badala yake ‘levo’ zao zipo kwa timu zenye majina makubwa yanayotikisa bara hili la Afrika.
Hilo limedhihirika wakati huu timu zinapopigana vikumbo kwenye zoezi la usajili ambapo Yanga wamekuwa wakigombea saini za wachezaji na timu kubwa ndani na nje ya bara hili, hiyo ikimaanisha kuwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara si watu wa mchezo mchezo kwa sasa.
Yanga wanajua kwamba wanakabiliwa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani na sasa wanaingia sokoni kwa nguvu ambapo wamejikuta wakigombea wachezaji na timu kubwa kama TP Mazembe ya Congo, Mamelod Sundown ya Afrika Kusini na baadhi ya timu za Uarabuni.
Mbali na timu hizo zinazowika katika bara la Afrika, pia wanajangwani hao wapo kwenye vita kali na moja ya timu kubwa nchini Israel ambayo inamtaka mchezaji wa Zesco ya Zambia, Jese Were, ambaye Yanga nao wanampigia hesabu kali.
Were ambaye ana rekodi ya kufunga hat-trick tatu katika mechi tatu mfululizo, anawaniwa na timu kadhaa na mbali na Were, pia Yanga wanapambana kutaka kumpa mshambuliaji wa zamani wa Azam, Kipre Tcheche anayecheza soka huko Uarabuni.
Timu hizo za Yanga, TP Mazembe, Sundown pamoja na timu hiyo kutoka Israel zikiwamo nyingine kutoka Uarabuni, zinagombea saini ya straika huyo huko Zesco, huku kila ikijitahidi kufanya linalowezekana kumpata huku Zesco nayo ikipambana kumbakisha kutokana na uwezo wake.
Mbali na Were, pia Yanga wapo kwenye vita kali kumnyakua kiungo mwenye uwezo mkubwa katikati ya uwanja, Misheck Chaila ambaye pia anaichezea Zesco.
Pia wanajangwani hao wameingia katika vita nyingine ya kuwania saini ya mshambuliaji, Thomas Ulimwengu aliyemaliza mkataba wake na TP Mazembe ambapo Mtanzania huyo anawindwa na timu zenye majina makubwa ndani na nje ya Afrika.
Wakati mabingwa hao watetezi wa ligi kuu wakihangaika kufanya usajili wa nguvu, nyuma yake wanayo kazi ya ziada kuwazuia mabeki wao wawili wa kati, Vincent Bossou na Vincent Andrew, ambao wanamendewa na timu nje ya Tanzania.
Hata hivyo, Yanga si mara ya kwanza kupambana na timu zenye majina kwani walishinda vita ya kumnasa kocha mpya, George Lwandamina ambaye Free State Stars ya nchini Afrika Kusini ilikuwa ikimfukuzia, huku pia Zesco nao wakitaka kumuongeza mkataba.
Wanajangwani hao wanataka kujiimarisha wakijua kwamba mwakani wanakabiliwa na mtihani mgumu klabu bingwa Afrika, ambapo wanataka kukamilisha zoezi hili mapema ili wamkabidhi kocha wao kila kitu, huku wakitaka kwenda kujichimbia moja ya nchi kubwa barani Ulaya kwa maandalizi.
Wakizungumzia taarifa hizo za usajili wa Yanga, baadhi ya wachambuzi wa soka wamesema kinachotakiwa ni kumwachia kocha majukumu yote, kwani yeye ndiye anayejua nani atamfaa na nani hatamfaa.
Kiungo za zamani wa klabu hiyo, Ally Mayai, alisema Wanajangwani hao wanatakiwa kujipanga mapema kutokana na ushiriki wao huo wa michuano ya kimataifa na kubwa wanalotakiwa kulifanya ni kumpa kocha ushirikiano wa kutosha, kauli ambayo inashabihiana na ya Kenny Mwaisabula.
Facebook Twitter

Makala ya awali
MESSI AZUA TAHARUKI CATALUNYA, AGOMEA MKATABA MPYA
Makala ijayo
MO amtia kitanzi Tshabalala

Bingwa
MAKALA KUHUSIANAZAIDI KUTOKA KWA MWANDISHI

‘Dab’ ya Pogba yatumika kufundisha wanafunzi Ufaransa

Msuva aanza kujifua kivyake

MO abebeshwa jukumu zito Msimbazi
HAKUNA MAONI
ACHA JIBU




UCHAMBUZI
Chelsea wampata mrithi wa Fabregas
Bingwa - November 18, 2016
Mashabiki Spurs wamlilia Isco
Bingwa - November 18, 2016
West Ham kumtimua Arbeloa
Bingwa - November 18, 2016
Mourinho anatamka staa wa Napoli
Bingwa - November 18, 2016
Rummenigge akiri Bundesliga imezidiwa kifedha
Bingwa - November 18, 2016

TUFUATILIE KUPITIA


HABARI ZAIDI

Chelsea wampata mrithi wa Fabregas
November 18, 2016

Mashabiki Spurs wamlilia Isco
November 18, 2016

West Ham kumtimua Arbeloa
November 18, 2016
KITENGO MAARUFU
Latest News1983
Habari1355
Sport Extra558
Burudani367
Makala250
Dondoo222
michezo kimataifa150
© Copyright New Habari (2006) Ltd
Designed by SMARTCODES
0 Comments