Simba imeamua kumtema kips wake Vicent Angban pamoja na mshambuliaji Frederic Blagnon.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kamati ya usajili na ya utendaji ya Simba kukaa na kukubaliana kabla ya dirisha la usajili kufungwa, kesho.
"Kweli hilo limefikiwa na huenda likatangazwa ndani ya siku moja," kilieleza chanzo.
Angban raia wa Ivory Coast ndiye alikuwa kipa bora wa mzunguko wa kwanza na alipoteza mechi mbili za mwisho za mzunguko huo.
Wakati Blagnon aliyewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Ivory Coast, naye amekumbana na panga hilo baada ya kushindwa kuonyesha cheche.
Sasa anaondoka na nafasi yake itachukuliwa na Mtanzania, Juma Luizio aliyekuwa akikipiga Zesco ya Zambia.
Tayari nafasi ya Angban imezibwa na James Agyei raia wa Ghana ambaye alikuwa akikipiga Medeama ya kwao Ghana.
0 Comments