Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TWITE KASAINI HAPA MCHANA HUU


Mbuyu Twite atua Majimaji


Mbuyu Twite

Kiungo mkabaji aliyemaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga, Mbuyu Twite yuko mbioni kutua katika klabu ya Majimaji.

Twite anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja leo baada ya mazungumzo kati yake na viongozi wa Majimaji kufikia pazuri.

Kocha wa Majimaji, Kally Ongala anamuhitaji Twite ili kuweza kumtumia katika kampeni ya kuinusuru na janga la kushuka daraja katika ngwe ya lala salama inayotarajiwa kuanza Jumamosi.

Majimaji imepania kufanya kweli baada ya kumsajili mshambuliaji wa Stand United, Kelvin Sabato Kongwe pamoja na kipa raia kutoka Cameroun Antorien Toukam



Posted via Blogaway


Post a Comment

0 Comments