Kiungo Mghana anayeaminika amekuja kujiunga na Simba kuziba nafasi ya Jonas Mkude, ametua nchini.
James Kotei ametua nchini leo saa 10:50 jioni akitokea kwao Ghana tayari kumalizana na Simba.
Mchezaji huyo kinda, anasifika zaidi kwa ukabaji na utoaji wa pasi ndefu anatarajia kumalizana na kusaini mkataba na Simba, kesho kwa kuwa mazungumzo ya awali yalishakamilika.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally 'Dizzo' ndiye aliyejitokeza kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kusema kwamba, baada ya mazungumzo ya mwisho kati yake na klabu hiyo kongwe, taarifa itatolewa.
0 Comments