Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kiiza arudi tena

Klabu ya URA ya nchini Uganda imemsajili mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga Hamis Kiiza kwa mkataba wa muda mfupi

Kiiza anarudi kwenye klabu ambayo ameichezea kwa miaka mitano ambapo amesaini mkataba utakaomuweka klabuni hapo hadi mpaka mwishoni mwa msimu kama ilivyo kwa mwenzake Emmanuel Okwi ambaye amesajiliwa kwenye klabu ya SC Villa kwa mkataba wa mfupi hadi mwishoni mwa msimu.

“Ni vizuri kurudi nyumbani. Nna kumbukumbu nyingi nzuri kwenye klabu hii na nimerudi kulipa fadhila ya imani waliyonionyesha.

Kiiza amekuwa akicheza kwenye klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini ambapo alijiunga mwezi Agosti akitokea Simba



Post a Comment

0 Comments