Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Madereva wa serikali kulipwa sawa na mtu mwenye elimu ya Digrii

Serikali imewaahidi madereva wake kuwa katika bajeti ijayo ya fedha ya 2017/2018, itatekeleza muundo mpya wa ngazi ya mshahara kwa madereva hao, ambapo sasa watakuwa wakipata kiwango cha mshahara sawa na mfanyakazi wa shahada ya kwanza.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na waziri wa nchi ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi Angela Kairuki, katika hotuba iliyosomwa na Afisa Tawala Mkuu katika wizara hiyo ya Utumishi wa Umma, Bw. Wilson Nyamanga.

Hata hivyo Afisa Tawala huyo amewataka madereva wa serikali kutimiza wajibu wao, kwa kuhakikisha suala la nidhamu linapewa kipaumbele wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Mapema katika risala yao, iliyosomwa na mmoja wa madereva wa serikali Bibi. Anna Mary Kaduma, madereva hao wameishauri serikali kulitafutia ufumbuzi tatizo la matumizi mabaya ya magari, linalofanywa na Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri mbalimbali, na hivyo kuwafanya madereva kufanya kazi katika muda wa ziada, bila ya malipo yoyote.



Post a Comment

0 Comments