Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Mayanga atangaza kikosi cha timu ya taifa ,Banda ,Kichuya ndani

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki.

Stars inaweza kucheza na kati ya Zambia na Rwanda au timu nyingine kwa kuwa kumekuwa na taarifa tofauti.

Lakini kikosi cha Mayanga kiliongozwa na nahodha Mbwana Samatta anayekipiga nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk kina vijana wengi zaidi.

Makipa;
Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Mabeki;
Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga), Mohammed Zimbwe ‘Tshabalala’ (Simba), Gardiel Michael (Azam), Andrew Vincent (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).

Viungo;
ni Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).


Washambuliaji;
Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden), Ibrahim Ajibu (Simba), Mbarak Yussuf (Kagera Sugar) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).
13
Mar
2017



Post a Comment

0 Comments