Mambo usiyoyafahamu kuhusu pesa taslimu:
1. Noti ndogo kuliko zote - Mwaka 1917 Benki Kuu ya Romania iliingiza sokoni noti yenye ukubwa wa stempu ya posta.
2. Noti kubwa kuliko zote - Mwaka 1998 Benki Kuu ya Ufilipino iliingiza sokoni noti yenye ukubwa wa karatasi la A4 kuadhimisha miaka 100 ya uhuru
3. Noti yenye tarakimu nyingi zaidi - Iliingizwa sokoni mwaka 2009 na Benki Kuu ya Zimbabwe na ina thamani ya Dola 100,000,000,000
4. Noti za Euro hufanyiwa majaribio kabla ya kuingizwa sokoni ili kupima uimara wake. Noti hizo zinatakiwa kuhimili maji yenye nyuzi joto 90, kukunjwa kunjwa au hata kumwagikiwa na maji ya kuondoa rangi ya kucha.
5. Noti za Euro 5 na 10 hutumika kwa wingi zaidi hivyo hutolewa kwenye mzunguko wa fedha baada ya miezi sita tu.
Tuambie nini unachokipenda au usichokipenda kuhusu pesa taslimu za hapa nchini whatsapp +25576660539
0 Comments