Hali yazidi kuwa tata, Korea Kaskazini yaunda kikosi maalumu cha kuikabili Marekani
Kwa mara ya kwanza na katika hatua ya kushadidi mvutano katika eneo la Peninsula ya Korea, serikali ya Korea Kaskazini imeunda kikosi cha operesheni maalumu.
Taarifa iliyotolewa na Pyongyang imesema kuwa, Kim Jong-un Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini ametoa amri ya kuundwa kikosi cha operesheni maalumu kwa ajili ya kukabiliana na hujuma tarajiwa ya Marekani. Hatua hiyo ni aina ya radiamali ya Pyongyang kwa hatua ya serikali ya Korea Kusini ya kuunda kikosi maalumu cha askari wa nchi hiyo na wale wa
Kikosi hicho cha nchi mbili kilichopewa jina la 'SEAL' kilishiriki kwa mara ya kwanza katika maneva ya hivi karibuni ya pamoja ya kila mwaka kati ya Marekani na Korea Kusini. Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Marekani sambamba na kutembelea mipaka ya kiraia kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini, amedai kuwa kipindi cha uvumilivu wa Marekani kuhusiana na Pyongyang kimefika mwisho. Mike Pence ambaye katika safari yake ya mara ya kwanza kuzitembelea nchi za Asia, amefanya safari nchini Korea Kusini na kuzungumza na waandishi wa habari kwamba, ili kufikia malengo yote na uhakika wa uthabiti wa raia wa Korea Kusini, Washington inachunguza machaguo yote kuihusu Korea Kaskazini bado yako mezani.
Miongoni mwa makombora hatari ya Korea Kaskazini
Katika hatua nyingine serikali ya Korea Kusini imetangaza kuwa, majarabio ya makombora ya Pyongyang yanahatarisha usalama wa dunia nzima. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini imesisitiza kuwa, hatua ya Korea Kaskazini kuonyesha makombora mapya katika siku ya jeshi nchini humo sambamba na kufyatua kombora jipya la balestiki, ni njia za kuonyesha uwezo wake wa kijeshi.
0 Comments