Header Ads Widget

Responsive Advertisement

tofauti ya kiisimu na kilahaja katika matumizi ya lugha

lugha





SWALI.
Kwa kutumia mifano kutoka katika lugha za makabila ya Tanzania, onyesha utofauti wa kiisimu na kilahaja katika matumizi ya lugha.             


Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kundi fulani kwa ajili ya mawasiliano. Lugha ni maneno pamoja na matumizi yake. (TUKI 2013).
Lugha; ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika
 MRISHO MPOTO NAPENDA KAZI ZAKO MJOMBA
mpango maalumu na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.
Lahaja ni tofauti katika matamshi, maumbo, na matumizi ya maneno katika maeneo mbalimbali kwa lugha yenye asili moja. (TUKI, 2013).
Lahaja ni vijilugha vinavyoibuka kwa lugha moja kuu kutokana na tofauti za kijiografia, kitabaka baina ya wazungumzaji wa lugha hiyo. Watu hao hutofautiana kimatamshi, muundo wa sentensi au msamiati.
Zifuatazo ni tofauti za kiisimu kutoka katika makabila ya Tanzania katika matumizi ya lugha:-
Lafudhi, hii ni tofauti mojawapo katika tofauti zinazojitokeza kwenye makabila ya Tanzania. Ile hali ya upekee wa mtu katika matamshi unaoathiriwa na lugha mama, mazingira yake ya kijiografia au ujuzi wake wa lugha inapelekea kutokea kwa utofauti. Mfano wasukuma lafudhi yao imejikita katika ukazaji wa maneno, kwa mfano neno ntakupiga silabi pihutamkwa kwa mkazo wa hali ya juu.
Kiimbo, ule upandaji na ushukaji wa sauti katika utamkaji wa maneno hutofautia katika kila lugha na kila kabila. Mfano mnyakyusa anaposema ugonile herufi uhutamkwa kwa sauti ya juu ambapo maneno mengine hutamkwa kwa kushusha sauti. Wakati huohuo wasukuma wanaposemamwangaluka neno mwa na kahutamkwa kwa sauti ya juu kuliko maneno ya kati. Hivyo kuna utofauti mkubwa sana wa kiimbo katika makabila ya Tanzania.
Mkazo, katika mkazo wa baadhi ya maneno katika utamkaji, makabila mbalimbali yanatamka kwa mtindo tofautitofauti. Kwa mfano kabila kama wakurya neno ninkutema nenote hutamkwa kwa mkazo sana kuliko maneno mengine. Lakini pia wanyakyusa utamkaji wao ni tofauti kidogo, kwa mfano neno ninkukomaneno ko hutamkwa kwa mkazo kuliko maneno mengine. Hivyo kuna utofauti mkubwa sana wa kiisimu katika makabila ya Tanzania.
Toni, makabila mbalimbali hutofautiana katika toni ambapo kila kabila lina toni yake katika utamkaji wa maneno. Kile kiwango fulani cha juu au cha chini cha sauti ndicho kinachotofautisha, mfano kabila la wahaya toni yao huwa ni ya chini ukilinganisha na toni ya wasukuma ambayo huwa ni ya juu. Wahaya katika neno zebilo(za siku) huwa na toni ya chini, wakati wasukuma nenojamashiku(za siku) huwa na toni ya juu. Hivyo kuna utofauti mkubwa wa kiisimu katika makabila ya Tanzania.
Utamkaji wa maneno, pia katika utamkaji wa maneno kuna utofauti mkubwa sana kutokana na makabila. Kwa mfano kabila la wahaya nenong’ombe wenyewe husema ngombe,lakini pia wakurya wametawaliwa sana na matumizi ya r, kwa mfano neno kula ambacho ni kitendo wenyewe husema au hutamka kura. Hivyo kuna utofauti mkubwa sana wa utamkaji wa maneno katika makabila ya Tanzania.
Msamiati, kila lugha ina utaratibu wake wa kujisimamia katika msamiati. Hii hupelekea kutofautiana kwa misamiati katika makabila hapa Tanzania. Kwa mfano neno makande hutamkwa kwa misamiati tofautitofauti kutokana na kabila lenyewe. Wasukuma husemamasangu lakini wanyakyusa husemaingati, hivyo kuna utofauti mkubwa sana kimsamiati.
Baada ya kuangalia tofauti za matumizi ya lugha kiisimu, ngoja tuone tofauti za kilahaja katika matumizi ya lugha. Hapa nitajikita zaidi katika kabila la wahaya na kabila la wazinza ambao wametenganishwa na ziwa Victoria:-
Msamiati, katika msamiati wazinza na wahaya hutofautiana sana. Katika Kiswahili kuna maji, wazinza husema amenzi na wahaya husemaamaizi. Pia neno kesho wazinza husema nyencha wakati wahaya husema nyenkya Hivyo katika msamiati kuna utofauti wa kilahaja kati ya wazinza na wahaya kwani kuna vijitofauti vidogovidogo vinavyojitokeza katika maneno yaani msamiati.
Sentensi, kuna tofauti ya kilahaja katika sentensi za kizinza na zile za kihaya.
Kwa mfano katika Kiswahili: mama amelala
                             Kihaya:  mai yanyamile.
                             Kizinza: maa yalyamile
Hapo tunaona katika sentensi kuna tofauti ndogondogo zinazojitokeza, mpangilio wa maneno upo sawa lakini tofauti ipo kwenye nomino maikwa wahaya na maa kwa wazinza. Na katika kitenzi yanyamile kwa wahaya, na yalyamile kwa wazinza.
Mofolojia, katika hii taaluma inayohusika na maumbo wazinza na wahaya hutofautiana kwa kiasi kidogo sana.
                      Kwa mfano: Kiswahili-anasoma
                                         Kihaya-nashoma
                                         Kizinza-nasoma
Kwa kuangalia mifano hiyo tunaweza kuona kwamba katika kutenganisha viambishi hufuata kanuni moja, kwa mfano kinapokaa kiambishi cha njeo kwenye kihaya ndipo pia hukaa katika kizinza isipokua hutofautiana katika mzizi. Kihaya mzizi ni shom na kizinza mzizi ni som.
Matamshi, katika matamshi wahaya hutamka maneno ya mwanzo kwa juu na kumalizia kwa kushusha sauti wakati wazinza hutamka kwa sauti iliyo lala.
                         Kwa mfano Kiswahili- jembe
                                            Kihaya- enfuka
                                            Kizinza-enfuka
Neno “e” kwa wahaya hutamka kwa juu sana na kumalizia maneno mengine kwa sauti ya chini sana, wakati wazinza hutamka kwa sauti ya kulala.
Kiujumla kila lugha inatofautiana na lugha nyingine katika Nyanja mbalimbali zikiwemo matamshi, maumbo, msamiati na maana ya maneno. Hivyo ni vizuri kwa kila watumiaji wa lugha(makabila) watumie lugha kutokana na eneo wanaloishi kwani kuna baadhi ya maneno yakitumiwa katika mazingira mengine hubadili maana. Asante msomaji wangu  powered by EMANUEL MASSHELE. 



MAREJELEO
Msanjila, Kihole, Massamba(2011): IsimuJamii Sekondari Na Vyuo. TUKI, UDSM.
TUKI (2013): Kamusi ya Kiswahili sanifu. Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
x

Post a Comment

0 Comments