Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WIZI WA MTANDAO :WATANZANIA WANAVYO IBIWA KUPITIA MITANDAO





UKWELI KUHUSU WIZI WA MITANDAO YA REVENUE BRUST, ONLINE TASK PAY, YOUTHNIZER BY GLORY MASSHELE Baada ya kupigiwa simu na watu mbalimbali akihitaji kujua uhakika wa pesa inayotangazwa kwenye mitandao ya OnlineTaskyPay, Money4Task na sasa Youthnize,

tumetafuta ukweli kuhusu hili. Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakuwa tayari umeshakutana na post hasa kwenye mitandao ya WhatsApp inayokutaka ubonyeze link fulani ili ujipatie hela. Unapojisajili tu unapewa Dola25 mitandaommingine unapata dola 10 na kadhalika ambayo kwa Tanzania ni takribani Elfu 60 kitu mabacho watu wengi wamekuwa wakijiingiza huko bila hata kujua hatma yake. Kwa uhakika mitandao hiyo ni ya uongo na ya kitapeli. Malengo ya mitandao ya namna hiyo ni kukupotezea muda, kuwatangaza wafahamike kwa kuwa traffic wanaoyipata kupitia link hizo huhamishwa kwenda kwenye tovuti ambazo baadae wanazifunua na hatmae kukuibia taarifa zako kama za anuani, barua pepe yaani e-mail na taarifa nyinginezo za kisiri. Kwa nini mitandao hii ni ya uongo na kitapeli? 1. Hakuna usalama wa kutosha kwa mtumiaji, mtu unajisajili kwa dakika 1 na taarifa zako ni email, username na jina la hundi (Cheque), kitu ambacho hakiwezekani kwa miamala ya kifedha. 2. Mtandao unohusika huwa ni mmoja tu ambao huwa unatumia majina tofauti tofauti mfano mwanzoni ulianza na jina la OnlineTaskPay, baadae ukabadilishwa na kuwa Money4Task na sasa unajulikana kama Youthnize. Lakini umeibuka tena mwingine unaoitwa Revenuebrast. 3. Ukishafikisha $300 au mingine mitandao wanataka dola 400 n.k. na kuendelea utahitajika uthibitishe kama wewe siyo roboti kw akubonyeza link fulani mbapo link hiyo haifunguki kamwe. 4. Malipo yote wanayatangaza kuwa hutolewa kuanzia tarehe 24-30 na usipofungua akaunti yako kwa siku 30 akaunti yako inafungwa. Muda huo wa malipo ukifika huwa wanabadilisha jina kama ambavyo nimeeleza hapo juu. 5. Muundo wa Mtandao yaani Dashboard au Homepage ina taarifa za aina moja na ndiyo ushahidi wakusema kuwa mtandao huo ni mmoja mabao unabadilishwha jina tu.Unawea kutazama picha kwa ushahidi zaidi wa mtandao huu. Japo muonekano wa mtandao wa sasa umebadilishwa kuliko ya zamani iliyotangulia. 6. Baadhi ya mitadao hiyo haina anuani ya ofisi zao yaani Physical Address kitu ambacho tumekizoea kwa matapeli wa mitandaoni. Uurasa wa OnlineTaskPay Huu ndio ukurasa wa mwanzo wa mtandao huo ninaouzingumzia. Matumizi ya ukuraza huu yalikuwa ni kwa mwezi wa 8 kuelekea wa 9. Anglia kwa makini muonekano wa homepage hii. Baada ya kufikia mwezi wa 9 kuelekea mwezi wa 10 Mtandao huo ulibadilisha jina lakini hawakubadilisha homepage yaani muonekano wa ukurasa wa mwanzo. Mwanzoni waliita OnlineTaskPay, hapo chini walibadilisha wakiita Money4Task. Tazam picha hapo chini. Ukurasa wa Money4Task Baada ya kufikia mwezi wa 9 mwishoni sasa wamebdalisha jina na kuuita mtandao huu Youthnize ambapo muonekano wa mtandao huu ni wa aina ile ile kama ambavyo unaweza kuona kwenye picha hapo chini. Ukurasa wa Youthnize Sasa mwanzoni mwa mwaka 2017 mtandao huu umebadilishwa na kuitwa Revenue Brust ukiwa na muonekano tofauti wa kuvutia kuliko ule wa mwanzo. Tazama picha hapo chini. Ukurasa mpya wa Revenue Brust Your Payment Withdrawal Option will appear here, when you will reach you minimum payout limit of 300$ You need [ 275 $ ] to get payout request form Kumbuka unapojisajili unatakiwa kuweka Email yako na hiyo ndiyo inyotumika kudukua taarifa zako ambapo ni rahisi hata kukuibia endapo baadae utaambiwa utoe namba yak oya bank ili wakutumie hela kitu ambacho wakati wa uchunguzi watu tumekishuhudia. Nini malengo hasa ya mitandao hii? Ni kweli kabisa kwamba malengo ya mitandao hii haina tija kwa mtumiaji. Lakini napenda kukili kuwa huenda kuna ambao wamelipwa hayo mamilioni ya bure kila mwezi. Hata hivyo tungependa kutoa fursa kwa ambao tayari wamelipwa watoe ushahidi kwenye sehemu ya comment kwenye blog hii ili wasomaji wajifunze zaidi. hakuna asiye penda hela tena ya kupata ukiwa umelala. Malengo amkubwa ya mitadao hii ni kuwanufaisha wanaomiliki mtandao na kuiba taarifa za mtumiaji. Wanafaidika vipi? Kwa kuwa watu wengu hutembelea mitandao hiyo, huwa inapata traffic kubwa ambayo baadae traffic hiyo huwamishwa kwenye site ambao hutengenezwa hivyo kufanyia biashara ya online advertisements ambapo huingiza kipato kikubwa kwa njia njia ya pay per impression/view yaani kitaalmu PPV. Mfano mzuri ni mtandao wa Youthnize ambao umekuwa website ya Intertainment iitwayo Youth Noize na kupata traffic kubwa kwa muda mfupi kwa kutumia traffic ya Youthnize ambayo watu wengi waliitembela kipindi hicho ukiwa ni mtandao wa mihela. Wanaibaje? Kupitia taarifa wanazokuomba ili wakulipe fedha kama umeshafikisha fedha tajwa kitaalamu inajulikana kama threshold huwa wanakuomba uwape namba za akaunti ya benki ili wakuingizie hela. Kadi lazima iwe ya kimataifa mfano Visa, MsterCard au American Express n.k. Hapo watakwambia uwape namba za kadi pia na namba 3 za mwisho za activation. hapo ndo mwanzo wa kuliwa unapoanza. Uongo kwa watumiaji. Watu wengi wanaotumia mitandao hii huwa ni waongo kwamba wamelipwa. Ukweli ni kwamba sisi hatuna ushahidi wa aliyelipwa. isipokuwa wtu wengi wanaowashawishi watu wabonyeze link zao huwa wanawambia kuwa wamelipwa kama njia ya kuwashawishi. Katika hali ya kawaida siyo rahisi fedha ya miaka hii ikapatikana kirahisi kiasi cha namna hii. Tufanye kazi Watanzania tusilimbuke na mitandao ya kijamii. Kama una swali lolote nitafute +255766605392 Nimewasilisha! MAELEKEZO YA MIONGONI MWA MITANDAO HII YAKO HIVI Member Guide: How do I promote my referral link? Promote your referral link on forums, blogs, comments, chat rooms, chats, facebook wall, facebook pages, groups, twitter, ptc sites, advertising websites to get link visits and earn money on every visit you sent through your link When will I get paid? The minimum balance required for payout is 300$ and you can get paid through PayPal, Cheque, Western Union, Money Gram, bank transfer at end of every month. How much can I earn? You can earn without any limits, it depends solely on your efforts and how much you work to promote your link. Many of our top members are earning more then 200$ per day and 5,000$+ per month This can’t be real. Are you giving free money? No, we are not giving away free money. We are paying you in order to generate traffic to our advertiser’s websites. We will get paid from our advertisers for the traffic we bring to them and paid commission to you people. Anti-CheatPlease note that we have a strong anti-cheat system, so do


Post a Comment

0 Comments