Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Israel: Wakati umefika wa kumuua Rais Assad wa Syria

Waziri wa Nyumba na Ujenzi wa utawala haramu wa Israel amesema wakati umefika Rais Bashar al-Assad wa Syria auawe kutokana na eti jinai anazowafanyia wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Yoav Galant, ameyasema hayo alipokuwa akihutubia waandishi wa habari nje kidogo ya mji wa Quds Tukufu unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu na kuongeza kuwa, kwa mtazamo wake, Rais Assad hana nafasi katika hii dunia na hafai kuachwa aendelee kuishi.
Waziri huyo wa Israel amesema kumuua Rais wa Syria itakua hatua ya kwanza ya kuikabili Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo imekuwa ikiiunga mkono serikali ya Damascus.
Kauli hii ya kichochezi inatolewa katika hali ambayo, hivi karibuni Marekani ilieneza habari za propaganda kuwa gereza la kijeshi la Saydnaya lililoko yapata kilomita 30 kaskazini mwa mji mkuu Damascus linatumiwa na serikali ya Rais Bashar al-Assad kuwateketeza moto maelfu ya wafungwa na raia wa kawaida waliouawa na vyombo vya dola, ili kuficha mauaji hayo, tuhuma bandia ambazo zimekanushwa vikali na Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria.
Wananchi wakiandamana kumuunga mkono Rais Assad
Yoav Galant, Waziri wa Nyumba na Ujenzi wa utawala haramu wa Israel amekariri madai yasiyo na msingi kuwa serikali ya Damascus iliua makumi ya watu kwa kutumia silaha za kemikali.
Hivi karibuni Marekani ilivurumisha makombora 59 ya Tomahawk kutokea meli zake mbili za kivita katika bahari ya Mediterania na kukishambulia kituo cha jeshi la anga la Syria katika eneo la Shayrat katika mkoa wa Homs na kuua watu tisa wakiwemo watoto wanne na kujeruhi wengine kadhaa, kwa kisingizio bandia kuwa serikali ya Rais Assad iliua watu zaidi ya 80 katika hujuma ya silaha za kemikali, suala ambalo lilikanushwa vikali na Damascus.
 +255766605392

Post a Comment

0 Comments