Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jihadul-Islam, yauonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel

Brigedia ya Quds tawi la harakati ya muqawama ya Jihadul-Islami ya Palestina sambamba na kuonyesha picha na video kuhusiana na mwendelezo wa siasa za sasa za utawala huo dhidi ya taifa la Palestina na Ukanda wa Gaza, imetoa indhari kali kwa utawala huo.
Harakati hiyo sambamba na kuonyesha kikosi chake cha walenga shabaha wa brigedi ya Quds kwa mnasaba wa kumbukumbu za tukio chungu la Nakbah dhidi ya Palestina ambazo huadhimishwa tarehe 14 Mei kila mwaka imeuhutubu utawala wa Kizayuni kwa kusema: "Kamwe msijaribu uwezo wa muqawama."

Wanamapambano wa Gaza

Mwisho wa kunukuu. Kadhalika umeionya Israel kukomesha ukandamizaji na mwenendo wake wa kupenda kujitanua zaidi na kusisitiza kuwa, ikiwa siasa hizo zitaendelea, basi Israel itakosa hata utulivu mdogo wa sasa. Wakati huo huo, Ramadan Abdullah Shalah, katibu mkuu wa harakati ya Jihadul-Islami ametangaza kuwa, ikiwa utawala huo katili utaendeleza mchezo wake mchafu dhidi ya taifa la Palestina, basi usitishaji vita wa sasa utafikia tamati. Kabla ya hapo, Fatha Hamad, mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa Haakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, alionya kuwa, muqawama wa Palestina sambamba na kuongeza uwezo wake wa kiulinzi, unaweza pia kutoa jibu kali dhidi ya uchokozi wowote wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwa kulenga kwa ustadi ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Askari wa Kizayuni wa Israel wakiwa wanalia baada ya kupigwa

Katika vita vya siku 50 dhidi ya eneo la Gaza, Harakati ya HAMAS ulishambulia maeneo ya jeshi la utawala wa Kizayuni kupitia njia za chini ya ardhi karibu na mpaka na eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments