Header Ads Widget

Responsive Advertisement

CANNAVARO: KWA MCAMEROON HUYU, KICHUYA HATUFUNGI


Nahodha na beki wa kati wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
SIKU chache tangu uongozi wa Yanga ukamilishe usajili wa kipa Mcameroon, Rostand Youthe, nahodha na beki wa kati wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameibuka na kutamka kuwa kwa kipa huyo waliyempata, basi Shiza Kichuya wa Simba hawafungi
tena. Yanga wiki iliyopita iliingia makubaliano kwa kumsainisha kipa huyo aliyekuwa anaichezea African Lyon iliyoshuka daraja msimu uliopita. Kutua kwa kipa huyo, kunamfanya aungane na makipa wengine Benno Kakolanya, Ally Mustapha ‘Barthez’ na Deogratius Munishi ‘Dida’ anayetajwa kwenda kucheza soka la kulipwa Sauz.
Akizungumza na Championi Jumatano, Cannavaro alisema kuwa, Youthe ni kati ya makipa waliokuwa bora msimu uliopita kutokana na uwezo mkubwa alionao. Cannavaro alisema, kipa huyo tofauti na uwezo wake, umbo lake kubwa linamsaidia kumuogopesha mshambuliaji yeyote na kupunguza ukubwa wa goli. “Msimu uliopita Simba
walitubahatisha kutufunga mabao rahisi ya mbali ambayo msimu ujao hawatatufunga tena kutokana na usajili wa bonge la kipa kutoka Cameroon. “Mimi sikuwa na taarifa za kipa huyo kusajiliwa, lakini kama ni kweli wamemalizana naye, basi wapinzani wasitarajie mteremko tena kutokana na ubora wake,” alisema Cannavaro. Msimu uliopita, katika mchezo
wa kwanza kati ya Yanga na Simba, Kichuya aliifunga Yanga bao la dakika ya 87 akipiga kona iliyoingia moja kwa moja na kufanya matokeo kuwa 1-1, na katika mchezo wa pili, Kichuya akaifunga tena timu hiyo bao la dakika ya 80 kwa shuti la umbali wa kama mita 20 na kuiwezesha timu yake kushinda 2-1.

Post a Comment

0 Comments