Na
Abdul Nondo.
Hii ni muhimu kusomwa na wazazi, wanafunzi ,wadau wa elimu na viongozi wote wa Taifa hili.
Nimesoma muongozo wa kuomba mkopo kwa mwaka 2017-2018,nilichokiona na kukisoma kama muongozo ni ujanja ujanja.
Muongozo ni kama maelezo ya mkataba wa ukopeshwaji kati ya bodi ya mikopo mkopeshaji na mwanafunzi mkopeshwaji.
Ila huwezi kuamini hakujawahi tokea muongozo wa ajabu na ujanja ujanja kama huu wa 2017-2018.ni muongozo wenye nia ovu ya kuwabana wanafunzi na wenye kuwapa nafasi wenyewe Bodi kufanya mambo kwa kufuata utaratibu wao binafsi, muongozo huu upo very general, vipengele vyote walivyoviweka katika muongozo wa mwaka juzi, mwaka jana ambavyo walivikeuka tukawabana wamevitoa hawajaviweka katika huu muongozo wa sasa,ambavyo ni vipengele muhimu na vya msingi katika makubaliano haya, na mkataba huu wa ukopeshaji.
1.Muongozo mzima ukiusoma hauelezi mwanafunzi specifically atalipwa kiasi gani, wameondoa hiki kipengele miongozo yote iliyopita ilikuwa ikionesha kuwa meals and accommodation (chakula na malazi) hutolewa sh. 8500 kwa siku kwa siku 60,sawa na sh. 510000/=,hela ya field miongozo iliyopita ilielezea sh. 10000/=kwa siku ndani ya siku 56 sawa na 560000/= ,hela books and stationary (BS).miongozo iliyopita ilikuwa inasema ni sh. 200000/=,huu ufafanuzi ulisaidia pale bodi walivyotoa fedha pungufu tofauti na muongozo WA mwaka jana ulivyo tulipinga waka kiri kosa wakasahihisha na wakafuata muongozo unavyosema.
Sasa tatizo lilipo muongozo wa sasa hautaji mwanafunzi atalipwa kiasi gani, kwa muda gani hivyo wamejiweka salama (safe )ili wakiamua kutoa kiasi chochote, elf 50 kwa miezi 2 sawa tuu, sababu hakuna pakuwabana na kuwauliza Ili baadaye wakitoa pungufu waseme *tuoneshe sehemu muongozo unapotuambia tukupe kiasi kadhaa*?
Haya waliyafanya mwaka Jana, ilitusiwabane wakakimbia kuondoa muongozo wao wa 2016-2017 na kuufutilia mbali mtandaoni hadi sasa haupo ukiutafuta, na walivyo keuka tulipoongea walisema *tuonesheni wapi boom na field haifanyiwi means testing*,bahati nzuri tulikuwa na Hard copies, sasa yote yaliyokuwa yanawabana wameyaficha na kuyaondoa ili wawe safe. (salama)
Kwanini wanafunzi wa post graduates waambiwe katika muongozo huu huu kuwa watalipwa kiasi kadhaa, ila undergraduates wasiambiwe?
Kwanini bodi wamekwepa kuweka hizi taarifa ambazo ni za msingi kwa mteja wao mwanafunzi anayekopa?.
2.Bodi hawa pia wamekuwa very General kusema,ukisoma muongozo wao wanasema muombaji ambaye mzazi wake *Business owners ambaye anatambulika na TRA (analipa REVENUE,KODI),na wamesajiliwa na mamlaka ya usajili wa biashara na makampuni ambayo ni BRELA expected not to apply, yaani *hawatarajiwi wala kutazamiwa kuomba mkopo*sababu wanauwezo.hayo maelezo ya bodi yanachanganya na hayana uhalisia.
sio kweli wote wenye biashara na kampuni zinazolipa kodi na zilizosajiliwa na BRELA wana uwezo wa kusomesha watoto vyuo vikuu kwa gharama zake, wengine wanalipa kodi, na wamesajiliwa ila mtaji wake ni pungufu ya gharama za kumsomesha mtoto chuo. Anzia ada, chakula kila siku, vitabu na hela ya photocopy, hela ya mafunzo kwa vitendo, hela ya malazi.
Bodi ingetakiwa kuonesha biashara ya ukubwa upi ya grossy income ya mwaka kiasi gani.
Pia, tuongee ukweli mbali na hayo, hata kuwa trace hao wafanyabiashara wakubwa, TZ hatuna huo mfumo wa data base, kwamba ukiingiza jina la mzazi wa mwanafunzi taarifa zake zitoke anafanya biashara fulani kiasi fulani ana gain sio rahisi ambao wanaweza kuwa traced ni watumishi wa umma tuu, ndio wengi wamesajiliwa na NIDA ndio wanaweza pata taarifa zao kama imeingizwa jina alilosajilia NIDA , hivyo hii inabakia ni uwaminifu wa Muombaji aandike taarifa za ukweli.
Ndio maana wamewatumia *are expected Not to apply* kuwapa hofu wasiombe kwa kuhisia hata pata, hii ni kwa sababu bodi hawananjia ya kuwatambua zaidi ya kupitia taarifa za muombaji, wangekuwa na huo uwezo wangeandika *are expected not to get, benefit* ,hata hao watoto wa vigogo wengine watapata tuu sababu hakuna njia rahisi ya kupata taarifa zao zaidi ya zitolewazo na waombaji, au labda mwanafunzi ambatanishe jina kamili lililosajiliwa katika kitambulisho cha NIDA, ila hawajasema kitambulisho cha NIDA katika muongozo wao, hivyo sio rahisi kuwa trace kupitia DATA BASE unaweza kuwa mtoto wa mwenye uwezo ukaomba na ukapata, hii ndio changamoto tuliyo nayo TZ.
03.Bodi ya mikopo hawajaeleza kwa undani juu ya MEANS TESTING, Means testing (MT) wameeleza ni njia wanayotumia kutoa mkopo kwa kulinganisha na ada ya O-level na A-level ndio wanapata jua wakupe sh. Ngapi au asilimia ngapi ,huwa inatumika katika Ada tuu, ndio maana Ada watu hupewa kwa asilimia tofauti tofauti mwingine laki 8,mwingine ml. Moja mwingine na nusu, ila chakula na malazi meals and accommodation, field, books and stationary huwa ni sawa 100% kwa kila mwanafunzi. 8500/= kwa siku wote
Sasa muongozo huu wa bodi 2017/2018 haujaonesha ,hiyo means Testing, itatumika wapi ada tuu, chakula na malazi (boom),au hela books and stationary, hapa ni mtego, unaowapa nafasi hata kutoa fedha ya chakula na malazi (boom) tofauti tofauti kwa kila mwanafunzi bila kufungwa na kipengele chochote kile.
4.kuhusu kukata rufaa (appeals) bodi ya mikopo imefumba macho hata kuelezea taarifa za msingi katika muongozo wao kuhusu kukata rufaa kwa watakao kosa, tumezoea miongozo ikitoa taarifa namna gani ya kukata rufaa kwa watakao kosa au kutoridhishwa na kiwango watakachopata watafanyaje, ni kiasi gani ,bodi imeshindwa hata kutoa hizi taarifa za msingi kabisa. Hii itapelekea wanafunzi wengi watakaokosa wakiwa na vigezo kutojua cha kufanya, kulikuwa na sababu zipi bodi kutoeleza taarifa za kukata rufaa?, ikiwa muongozo huu ndio mawasiliano makubwa Kati ya bodi na wanafunzi.
Sioni dhamira ya dhati ya kuwasaidia wanafunzi kusoma elimu ya Juu, ila naona kukomoana, na kuwindana kati ya bodi na wanafunzi.
Bodi wanajijali saana wao ndio maana muongozo umeacha taarifa za msingi kwa mwanafunzi na kujikita saana kuelezea namna ya kulipa Deni.
Hii ni ishara ya wazi serikali kupitia bodi ya mikopo imeanza liking'atua kugharamikia elimu ya juu, haya ndio madhara ya *cost sharing policy* ilioanza mnamo mwaka 1990's ambapo tulishuhudia viongozi kama *James Mbatia* *Chacha zakayo wangwe*, *Anton komu*,zitto zuberi kabwe na wengine walipinga serikali kujiondoa kugharamikia elimu.
Na sasa serikali za wanafunzi zimekuwa kimya, pia taasisi za elimu zimekuwa kimya kusemea. Mambo kama haya yanapotokea.
Mungu awabariki na awaongoze ila wanafunzi wote msiache omba mkopo kama hali ya kiuchumi sio nzuri,
Idara yetu kupitia mtandao wa wanafunzi Tanzania, tunaangalia namna gani ya kulisemea Hili.
Abdul Nondo.
0659366125
Kaimu mkurugenzi Haki na wajibu wa wanafunzi (Mtandao wa wanafunzi TANZANIA-TSNP)

0 Comments