RAFU YA BODI YA MIKOPO PART 2,DHIDI YA WAOMBAJI WA MIKOPO.
Na
Abdul Nondo
Naomba nitumie muda na maneno machache dhidi ya bodi ya mikopo,kutokana na taarifa aliyoitoa mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul Razack Badru,kuwa kuna wanafunzi wamekosea kujaza taarifa zao,wameenda kinyume na maelekezo ya muongozo wao.
Labda Mimi niseme kitu kuwa sioni nia ya dhati ya bodi kutoa mikopo kwa wanafunzi hawa,hata hao wenye uhitaji naona kuna zengwe linatengenezwa ili wenye kasoro wawe wengi zaidi,ili idadi yao ya watu 30000 kupewa mikopo iwe fixed,yaani wasitoe zaidi ya hao ikiwa waombaji hadi juzi tarehe 29 ilikuwa zaidi ya waombaji 49000.
Kwa nini nasema hivi?
1.ukisoma huu muongozo wao wa 2017/2018,namba 7 wanasema utakapoomba huwezi pata nafasi ya kurekebisha taarifa zako ,kwanini utaratibu mwaka huu ubadilike wanafunzi wasipewe nafasi ya kurekebisha taarifa zao?
Ikiwa mkurugenzi tayari amesema wapo waliokosea,je hatima yao ni nini?.
Hapa tuelewe kuwa muda ulioongezwa na bodi hiyo hadi sept ,11 sio muda wa marekebisho hata kidogo,ingawa mkurugenzi alidai muda huo ni kwa ajili waliokosea wakarekebishe,hapana sio rahisi mwanafunzi kujua kama wamekosea isipokuwa hadi majina yao yaoneshwe mtandaoni na bodi kuwa wamekosea taarifa zao,kama ilivyokuwa zamani.
Muda ulioongezwa ni kwa ambao walikuwa hawajamaliza kuomba ,tuelewe mtandao ulikuwa unasumbua,wengine control number walikuwa hawajapewa ingawa walikuwa wamelipia,hivyo muda huu ni kwaniaba yao ,na sio kwa waliokosea,kwa waliokosea bodi tayari imesema haina muda wa kutoa ili wanafunzi warekebishe taarifa zao.
Ndugu,zangu hili hatuwezi kuliunga mkono tunahitaji bodi watangaze majina ya waliokosea mtandaoni wajione,warekebishe kwani makosa mengi yanasababishwa na bodi wenyewe.
Katika muongozo wao bodi walisema wanafunzi wanaweza Ku attach other documents, (nyaraka zinginezo) mfano ,nyaraka zinazoonesha kudhaminiwa,lakini katika mfumo wao wa OLAMS (online application and management system)Hakukuwa na sehemu ya kuambatanisha other documents, kama nyaraka ya udhamini ,ila cheti cha taaluma,kuzaliwa,kifo hakukuwa other document kama nyaraka za kudhaminiwa.
Hadi tarehe 29 August, ndio walikiweka hiki kipengele cha other documents attachment. why ?.
Hawa waliambatanisha tuu bila Ku upload
Why,bodi walisahau au walikosea ?,kwanini wanafunzi wasikosee kama bodi wenyewe wanakosea.
Pia katika work status (kazi ya mzazi au mlezi) bodi waliweka options za kazi ,unachagua waliweka kazi kubwa kubwa ,engeering,mfanyabiashara,waliweka kazi zao wewe unachagua (peasant)mkulima hawakuweka ,baada ya wiki 2 ndio walikuja badili kuweka hiyo peasant,je bodi walisahau? Au waliokosea ? ,kama walisahau au kukosea kwanini mwanafunzi asikosei au kusahau kama bodi wanakosea?
Mfumo wa bodi sio rafiki,mfumo wa kuomba uki command huruhusiwi tena kurekebisha ,bodi wangeweza kutengeneza mfumo ambao Akaunti ya muombaji ingekuwa wazi hadi mwisho wa muda yaani(deadline) kuwa awe na uwezo wa kubadili CONFIRM and UNCONFIRM vipengele hivi vingekuwepo ingesaidia hadi mwisho ,wa muda ndio wakafunga ila sijui bodi kama walisahau au walikosea,kama WALIOKOSEA kwanini mwanafunzi asikosee.
Huwezi mnyima mtu mwenye uhitaji kwasababu tuu alikosea kipengele Fulani katika fomu hiyo.
TUNAOMBA BODI YA MIKOPO WATOE MAJINA MTANDAONI WAZI ,DHAHIRI YA WALIOKOSEA ILI WAPEWE UTARATIBU WA KUREKEBISHA TAARIFA ZAO MUDA UNATOSHA.
Abdul Nondo.
Kaimu mkurugenzi idara ya
Haki na wajibu wa wanafunzi.
Mtandao wa wanafunzi Tanzania.
0659366125.

1 Comments
Ni sahihi kabisa kwasababu hatujui ni wapi tumekosea.Nivema bodi itangaze majina ya walio kosea na kutaja vitu au kitu kilichokosewa ili kiweze kufanyiwa marekebisho.
ReplyDelete