Watu wengi tumekuwa na kiu au shauku ya kuwa na kumiliki vitu vya gharama.
Mwanafunzi shuleni hutamani kuwa na Alama za juu kabisaa Mfanyakazi anatamani kupanda cheo au kumiliki kampuni yake. Mrembo atatamani kuvaa na kupaka vitu vya gharama Mfanyabiashara anatamani kuongeza biashara yake na kupata faida kubwa
Vitu vyote hivi vina gharama na iwapo MTU atavipata basi atapata heshima, hadhi ,na thamani kwake na kwa watu wanaomzunguka
Lakini jambo moja linalofichika katika vitu vya gharama ni GHARAMA. Ili kupata vitu vya gharama lazima uhakikishe unalipia gharama ya hivyo vitu
Hivi fikiria MTU mwenye uzito uliozidi anatamani kupunguza uzito wake lakini wakati huohuo hataki kupunguza vyakula vyenye mafuta, hataki kufanya mazoezi wala kufuata utaratbu mzuri Wa kula . Mtu kama huyu kupungua itabaki kuwa ndoto na matamanio tyuuu
Ndivyo ilivyo kwa kila kitu cha gharama lazima ukubali kujigharamia. Hakuna namna nyingine ya kuepuka gharama hizo.
Ukipata vikwazo usihesabu Kama changamoto ila jikumbushe tuuu “NAJIGHARAMIA "
Leo kubali kugharamia Biashara yako
Gharamia elimu yako
Gharamia mahusiano yako
Gharamia afya yako
Gharamia familia yako
Gharamia ndoto yako
Matunda ya gharama utakazolipa Leo ni gharama utakayoivuna kesho
0 Comments