Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kikosi cha wasanii wa Bongo Fleva wanaosakata soka hiki hapa



Kama sio kufanya kwake vizuri kwenye muziki basi huenda msanii, Alikiba ‘King Kiba’ angejikita kwenye utafutaji wa maisha ya soka.
Alikiba ni mwana michezo ambaye mara kadhaa amekuwa akijihusisha na soka, anauwezo wa mzuri wa kutumia mguu wake wa kushoto na kipindi cha nyuma alikuwa  anaichezea  Mwiba, Kariakoo.
Msanii huyo pia ni shabiki wa kutupwa wa Yanga, ni mmoja pia wa mashabiki wa timu hiyo ambaye aliumizwa na kuondoka kwa Haruna Niyonzima.
Mbali na King Kiba ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa Seduce Me wapo wasanii wengine ambao nao kama sio muziki wangekuwa kwenye soka.
Wasanii hao ni Young Killer “Msodoki”, Harmonize, Stamina, Hussein Machozi, H Baba na hata mdogo wake na Ali Kiba ambaye ni Abdul Kiba.

Post a Comment

0 Comments