Tunaishi kwenye ulimwengu unaotegemeana .Hivi umeshawahi kugundua kuwa hata miti hutegemea watu ili ijitengenezee chakula. Hebu tafakari kuhusu mwili wako Leo kichwa kinabebwa na shingo, mikono inashikiliwa na mabega, miguu inaubeba mwili wote hata damu hutegemea moyo kusukumwa na kuchujwa ili ifae kwa matumizi ya mwili.
Utegemeano huu wa mwili unashangaza Sana'a haswa pale unapogunduwa ikiharibika sehemu moja basi na mwili wote hupata udhaifu.
Hivi ndivyo ilivyo kwenye dunia kila mtu ana nafasi yake kwenye maisha ya mwingine. Tuwatathimini watu hawa
Mwalimu anamuhitaji Daktari kwa ajili ya afya yake lakini pia Daktari anamuhitaji mwalimu ili apate ufahamu wa kutibu
Mmiliki wa mtandao wakijamii anamuhitaji mtengeneza vifaa vya kielektroniki Kama vile simu na kompyuta ili kuuza Huduma yake na wakati huohuo mmiliki wa vifaa hivyo humuhitaji mmliki wa mtandao wa kijamii ili kuongeza thamani ya bidhaa yake
Leo tujaribu kujichunguza jinsi gani tunaweza kukamilisha maisha ya mtu mwingine na tuishi kwa kusaidiana maana hii ndo kanuni ya dunia
Ukiweza kumfanya mtu acheke Leo Fanya hivyo bila kusita Kesho yupo atakaye kuchekesha na wewe pia
0 Comments