Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kutokana na mpasuko wa kisiasa nchini Hispania sasa Barcelona wanaweza kuanza kucheza ligi kuu ya Epl



Wakazi wa Catalunya wanataka kuwa huru, uhuru ambao utawafanya kujitenga na taifa la Hispania. Catalunya itakuwa Catalunya na Hispania itakuwa Hispania.
Kama suala hili likapitishwa baasi moja kwa moja litakuwa na athari na ligi kuu nchini Hispania La Liga kwani timu zinazotoka Catalunya zikiongozwa na Barcelona hazitakuwa sehemu ya La Liga.
Hii imezua maswali mengi sana miongoni mwa mashabiki wa La Liga haswa ukizingatia kwamba Catalunya ukiacha Barcelona pia zipo Espanyol na Girona.
Waziri anayehusiana na masuala ya michezo nchini Hispania Gerard Figuares ametoa tamko kuhusu nini kinaweza kutokea kwa timu za Catalunya pia akitoa uwezekano wa timu hizo kwenda kukipiga Epl.
Figuares amesema Barcelona,Espanyol na Girona wanaweza kuamua wapi wanataka kwenda kucheza, wanaweza kucheza ligi ya Hispania au ligi za nchi jirani kama Uingereza na Ufaransa.
Hii inaweza kumfanya Lioneil Messi kuanza kukipiga Epl huku pia mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Luis Suarez akirejea tena katika ligi kuu Uingereza.

Post a Comment

0 Comments