Kaimu Rais wa klabu ya soccer ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, Salim Abdallah amesema maandalizi yote kuelekea kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Al Masry ya kombe la Shirikisho Afrika yamekamilika na kilichobaki ni dua zao Watanzania.
Akizungumza na kipindi cha Mshikemshike kinachorushwa na kituo cha luninga cha Azam, Salim amesema wanatambua wanakikosi bora lakini hawawezi kupata ushindi kama tu hawatajituma katika mchezo huo.
"Tupo huku kufanya kazi, Mungu akipenda Jumamosi watu wategemee matokeo mazuri, sina wasiwasi na vijana, tumewaandaa vizuri na wanamorali ya kutosha Mimi nadhani ni dua tu tunahitaji," Abdalah amesema.
Abdalah amesema wanakiamini kikosi kutokana na mafunzo mazuri wanayoyapata kutoka kwa benchi la ufundi likiongozwa na kocha Pierre Lechantre.
"Naamini tunakikosi bora, lakini kikosi bora hakiji hivihivi kinahitaji ufundi, kinahitaji uweledi ndo maana tulimchukua mwalimu huyu, ameongeza thamani kwenye kikosi ona hata tunavyocheza, sasa Simba ni moto wa kuotea mbali" amesema.
Simba wapo mjini Port Said nchini Misri kwa maandalizi ya awali kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika kwenye uwanja wa Port Said Jumamosi Machi 17.
Katika mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es Salaam mabao ya John Raphael Bocco na Emmanuel Okwi yaliifanya Simba kutoka sare ya mabao 2-2 hivyo wanahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili kusonga mbele.
Waamuzi wa mchezo huo
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea ambapo Mwamuzi wa kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin.
Kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.