Ni wazi kuwa kila mtu katika dunia alizaliwa na wazazi haijalishi ni kwa njia gani ila lazima kuna wazazi waliotuleta duniani. Wazazi hawa ni tunu ambayo ni ya thamani sana. Wakati tukiwa watoto wazazi wanabeba jukumu kubwa kututengeneza na kutulea ili tufike hatua tunayoitamani.
Ni Mara ngapi ulishakaa na wazazi wako na kuwauliza juu ya magumu au hata nyakati za huzuni na furaha walizopitia wakati wa kukulea hadi ulipofika!!?? Kama hujawahi kufanya hivyo jaribu kufanya hivyo Leo!
Kikubwa nachotamani kukushirikisha Leo ni namna tunavyothamini uwepo wa wazazi wetu ( mzazi si lazima aliyekuzaa Yoyote aliyebeba jukumu la uzazi na malezi ni mzazi) .
Tafakari mwenyewe ni Mara ngapi umetoa muda, Mali na kitu chochote cha thamani kwa ajili ya wazazi wako. Katika ulimwengu huu ni rahisi kuona MTU akinunua zawadi ya thamani kubwa kwa ajili ya rafiki au mpenzi wake. Ila ni Mara chache mno MTU kufanya hivyo kwa wazazi wake. Tunasubiri siku ya mama au baba au siku za kuzaliwa ndo tuwaweke kwenye mitandao ya kijamii ambayo hata wazazi wetu hawaijui wala kuitumia wakati mwingine.
Mara nyingine tunajidanganya na kauli Kama hatuwezi kuwalipa wazazi! Au hakuna kinachofikia upendo na malezi yao! Ni kweli hatuwezi kuwalipa na hatupaswi kuwalipa lakini ni lazima kujitoa kwa ajili yao. Hebu jiulize ni Mara ngapi uliwakumbuka wazazi wako katika bajeti zako za fedha!??? Au unaona fahari kula vyakula vizuri, kuvaa mavazi ya thamani kujivinjari na marafiki zako kwenye hotel za kifahari na wakati wazazi wako wanateseka?? Unaona ni sifa kununua vocha kuongea na marafiki zako masaa au siku nzima na unashindwa kumpigia simu mzazi wako ukaongea nae kwa dakika mbili tuu ?? Hata Kama wazazi wako wanajiweza au ni matajiri wanatamani kupata angalau zawadi kidogo tuu kwako. Wanatamani kupokea simu zako, mara nyingine wanatamani kusikia ukiwasifia kana unavyowasifia marafiki zako. Unaweza kufanya kazi kwa bidii, kusoma Sana'a, kutafuta Sana'a ila bila Baraka za wazazi ni ngumu Sana'a kufanikiwa.
Hatukatai kuna mambo ya kuumiza tumeshawahi kufanyiwa na wazazi ila hayalingani hata kidogo na Yale mema waliyotutendea. Hata maandiko matakatifu yanasema tuwaheshimu wazazi ili tupate Baraka na heri.
Unataka baraka na heri ???
Waheshimu, wapende, wathamini, wakumbuke na kuwaombea wazazi wako. Kuwaweka kwenye mitandao ya kijamii haitoshi . JITOE kwa ajili yao.
