Simba itakuwa inashuka dimbani kukipiga na mashetani hao ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa awamu ya kwanza kumalizika kwa kufungwa mabao 2-1 ugenini.
Kuelekea mechi na Nkana, Simba leo itakuwa na kibarua cha ligi kucheza na KMC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipute cha leo na KMC kimefanya Mbelgiji Aussems kubadili aina ya wachezaji ambao atawatumia ili kuwapa nafasi wale nyota Jumapili dhidi ya Nkana.
Imeelezwa kuwa Mbelgiji atawatumia wachezaji wengi zaidi ambao hawachezi katika kikosi cha kwanza kwa hofu ya kutoumia kabla hawajakutana na miamba hiyo ya Zambia.
