Header Ads Widget

Responsive Advertisement

UHAKIKI TAMTHILIYA YA MALKIA BIBITITI MUHAMEDI, NAFASI YA MWANAMKE NA MASUALA YA KIJINSIA NA EMANUEL MBOGO


Tamthiliya ya Malkia bibititi MUHAMEDI  imeandikwa na profesa Emanuel Mbogo
Ni tamthiliya inayo elezea harakati za kudai Uhuru zilizokuwa zinafanywa na Biti titi pamoja na wahusika wengine. Mwandishi kwa kiasi kikubwa amemkweza mwanamke kwa kuonekana kuwa ni jasiri, mvumilivu, anayejituma, mwenye mapenzi ya kweli na nchi yake, nk .pia mwanamke ameonekana kama msaliti akimtumia mhusika Hadija aliye ingilia ndoa ya Boi na mkewe Titi , vilevile Mwandishi ameonesha changamoto wanazokumbana Nazo wahusika wanawake katika harakati za kudai Uhuru mfano Bibititi alifungwa Gerezani kule Dodoma , pia Mwandishi anonesha jinsi Tatu alivyo achwa na mumewe kisa harakati zake za kudai uhuru.

Mwanaume katika tamthiliya hii anaonekana kama msaliti na asiye weza kuvumilia pindi mke wake hayupo.

Aidha kwa namna Fulani katika tamthiliya hii kulikuwa na ushirikiano kati ya mwanaume na mwanamke , hapa tunaona jinsi Bibititi alivyo shirikiana na Nyerere katika ukombozi

Masuala ya kijinsia yanayo jadiliwa na Mwandishi ni
Ndoa, mgawanyo Wa majukumu, unyanyasaji, ushirikiano na maswala mengine.

Mwandishi anaonesha kuwa wanawake wanaweza kufanya mapinduzi katika Jamii.
Aidha Mwandishi huyu anamtazama mwanamke kwa namna chanya zaidi.

Na Emanuel Mashele
Info.masshele@gmail.com

Post a Comment

0 Comments