Header Ads Widget

Responsive Advertisement

UTATA WA MWANAMKE KATIKA USHAIRI WA KISASA

MWANAMKE ANGALI TATA KATIKA USHAIRI WA KISASA?



Kwanza yafaa tujue maana ya utata,
Utata ni hali ya kutokueleweka , kiumbo, kifikra, kijinsi, kijinsia, kimtazamo, au kimazingira, kwa namna moja isiyo na shaka.

"Je mwanamke angali tata katika ushairi Wa kisasa?

Hili ni swali alililojiuliza Florence Indeede yenye kichwa hicho hicho cha habari.
Kabla ya kuandika makala yake anasema kuwa alitarajia kukutana na umbo jipya la mwanamke katika ushairi Wa kisasa.
Mwandishi ana sema kuwa "Uhakiki huu umechochewa na mjadala aliowahi kuuzwa Said Ahmed Mohamed mwaka wa 1984

katika Kina cha Maisha kwenye Shairi – Mwananamke (uk. 18), lenye kibwagizo “Mwanamke ali

tata, tata tulitatulile.” Ni miaka mingi ambayo imepita tangu kuzua swala hili na ndiposa wasilisho

hili linatizama utata wa mwanamke katika mashairi (mazingira) ya kisasa. Tahakiki nyingi

zinaonyesha kwamba swala la mwanamke katika ushairi liliangazia sana Utenzi wa Mwanakupona

ulioandikwa kabla ya karne ya kumi na tisa. Ni dhahiri kwamba katika karne ya ishirini na moja,

washairi wengi wameibuka na sanaa na mitindo mbali mbali ambayo inamsawiri mwanamke kwa

namna ya kumkweza ama kumtweza kwa matumizi ya jazanda na mitindo mbalimbali ya lugha.

Tunatetea kauli kwamba washairi wa kisasa wana nafasi bora ya kumjenga mwanamke kwa njia

chanya zaidi hasa ikilinganishwa na washairi awali ambao utamaduni wao ulimtweza mwanamke

asemavyo Said Ahmed Mohammed (1984): “Mwanamke ali tunda, ladha yake ili

tamu…Mwanamke ali tata tata tuitatulile.” Ni katika muktadha huu ndipo tunachukulia kwamba

matini za kishairi za kisasa zinahusisha mbinu na nyenzo mpya ambazo zimebadilisha sura na

taswira ya mwanamke. Maswali yanayoibuka ni; Je, Mwanamke angali tata katika ushairi wa

kisasa kwenye enzi ya karne ya ishirini na moja? Je, ni kwa kiwango gani washairi wa kisasa

wamelitatua swala hili, akiwemo Said Ahmed Mohammed mwenyewe? Je, umbo jipya la

mwanamke ni lipi katika ushairi wa kisasa? Katika kujibu maswala ibuka haya uhakiki huu

utachunguza ushairi wa Said Ahmed Mohammed, zikiwemo diwani za Jicho la Ndani (2002),

Kithaka wa Mberia, Bara Jingine (2001), na mashairi katika Diwani ya Karne Mpya (2007)

miongoni mwa nyingine. Ni matumaini yangu kwamba wasilisho hili linatoa mchango mkubwa

wa mjengo upya wa taswira ya mwanamke kama nyenzo mojawapo ya kutimiza malengo ya

millennia na maono ya 2030
Aidha mwandishi Wa makala hiyo ya mwanamke angali tata katika ushairi Wa kisasa anadai kuwa " Ufalsafaji na matumizi ya ushairi pamoja na tashibiha katika ushairi ndicho chanzo cha utata katika swala la mwanamke.
Pamoja na hayo ukweli nikwamba utata Wa kuchambua dhana ya mwanamke inazidi kuangaziwa na watunzi na wataalamu mbalimbali katika mikondo ya kifasihi. Hivyo utaona kuwa pasi na umbo la mwanamke, maisha take, visa na mikasa , pilikapilika , maudhi na changamoto anazo kumbana Nazo mwanamke ni mchanganyiko Wa utata unao washinda watu kuelezea kuhusu kiumbe huyu Wa ajabu.
Mwandishi Wa makala Florence anadai kuwa "utata huu unao mrejelea mwanamke , kama pambo na maumbo mengine ya ajabu ndilo swala linalo ongelewa na Said Mohammed katika ushairi la " Mwanamke".
UANAMKE KATIKA LUGHA YA KISHAIRI:

Ukipata wasaa wakupitia tungo za ushairi kadhaa za SHARBAN ROBERT NA SAID MOHAMED
utaona mwanamke anafananisha na pambo la kiulimwengu au Ua
Mwanamke anafananishwa na kifaa na matumizi ya mofu ya "li"
"UA la ngu nalipenda" na swala hili limeishi tangu kale tangu enzi za " utenzi Wa mwanakupona"
hadi katika zama hizi za maendeleo ya tehama.
Fluornce katika makala yake anasema "pamoja na mabadiliko na harakati za kumkombo mwanamke kutokana na mtazamo hasi bado mwanamke angali katika utata"  kama utapata wasaa wa kupitia katiba yakenya kwenye maswala ya jinsia utaona mwanamke anatajwa kuwa na haki sawa na mwanaume tunaita fiftyfity. Lakini pamoja na hayo dhana hiyo imebaki ni propaganda tuu.
Aidha Florence anadai kuwa wasanii Wa sasa na waiopita wamedhihitisha utata Wa mwanamke ama Wa jadi ama Wa kisiasa.
Mahitimisho.
Utata katika ushairi Wa kisasa katika kipindi hiki cha harakati za kumkomboa mwanamke unasababishwa na kutaka kumkweza ama kumtweza mwanamke .
Huenda ukashangaa nivipi kumkweza mwanamke kunaleta utata kwa mwanamke. Ukweli nikwamba mwanamke wakati mwingine amepewa uwezo Wa ajabu mno hadi kuushinda uhalisia. Mwanamke anapewa majukumu mazito, na uhusika Mzito kitu ambacho kinazidi kumwongezea utata kiumbe huyu
Lakini swali la kujiuliza hapa ni kuwa je kama mtunzi wa ushairi kaiota kazi hiyo je niyeye ndiye mwenye kumsababishia utata mwanamke? Au jamii ndiyo inayo msababishia mwanamke utata? Au kiuhalisia mwanamke ni kiumbe tata? Na kuwa wasanii wanausawiri utata huo katika tungo zao.

Mchambuzi Wa makala hii ni mtaalamu Wa lugha na Fasihi pia mwandishi Wa makala za kiswahili&Tehama.
Info.masshele@gmail.com

Post a Comment

0 Comments