Katika kuhakikisha Mdau wetu hipitwi na chochote, hasa kuhusiana na kiswahili mtandao huu umewasiliana na ubalozi Wa Tanzania nchini Africa kusini kutaka kujua , baada ya serikali ya afrika kusini kuridhia kuanza kufundishwa kwa somo la kiswahili nchini humo, ofisi ya ubalozi Wa Tanzania Pretoria , imejipanga vipi kuhakikisha fursa za kufundisha lugha hiyo katika nchi ya afrika kusini inawafikia watanzania nasio nchi nyingine kama Kenya Uganda n.k
Ofisi ya ubalozi ilikuwa na haya yakujibu
Bw Emmanuel Mashele
Salaam
Ubalozi umepokea barua pepe yako inayotaka kujua ubalozi umejipanga vipi ili fursa ziwafikie Watanzania.
Ubalozi upo katika mazungumzo na Serikali ya Afrika ya Kusini kuhusu suala la Kiswahili. Utaratibu uliyopo katika Serikali ya Afrika ya kusini ni kuwa ukileta Lugha yako lazima ugharamie mahitaji yote( Kulipia Walimu,Mitaala, Vitabu) ili lugha hiyo ifundishwe katika shule za Afrika ya Kusini. kama lugha za Tamarin, Kifaransa, Kichina, Kijerumani n.k
Lakini kutokana na mashirikiano yaliyopo kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika ya Kusini wanapanga kuleta waaalimu wao kuja kujifunsa Kiswahili maana Kiswahili kitakuwa kinafundishwa kama lugha ya pili na siyo lugha ya kwanza.
Aidha, pale fursa za walimu wa Kiswahili zitapelekwa katika Wizara ya Elimu Sayansi na Vyuo vya Ufundi.
Rosemary Chambe Jairo
Pretoria
Natumaini sasa umeelewa kila kitu , usisahau kuacha comment yako ili baadaye mheshimiwa ubalozi akipita aione.

0 Comments