Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TANZANIA WATAFUZU AFCON JUMAPILI


Na info.masshele@gmail.com
Kundi L, mpaka sasa timu zote nne zina nafasi ya kufuzu michuano ya Afcon.

Kundi hilo linalo ongozwa na Uganda yenye pwenti 13, tayari wamesha fuzu huku Tanzania na Lesotho wakiwa na pwenti 5, Aisha Capeverde wanashika mkia na pwenti zao 4.

Hivyo baada ya Uganda kufuzu , timu zilizo bakia ambazo ni Tanzania , Lesotho na capeverde wanawania kushika nafasi ya pili katika kundi ili kuungana na wababe Uganda kwenda Afcon.


MSIMAMO
  • 1   Uganda 13

   Tanzania  5


   Lesotho5
 Capeverde 4


Hesabu ziko hivi
Kama Tanzania ikimfunga Uganda halafu mchezo kati ya Capeverde na Lesotho umalizike kwa sare au Capeverde ashinde basi Tanzania tashika nafasi ya pili na atakuwa amefuzu.

Sare kwa mchezo kati ya Tanzania na Uganda itakuwa faida kwa Lesotho kama akipata sare au kushinda katika mchezo wake Wa ugenini dhidi ya cape Verde , vile vile kama Tanzania atapata sare ama kufungwa halafu Capeverde ashinde basi ataungana na Uganda katika michuano ya Afconi.

TANZANIA NA UGANDA
Mchezo huu hauwezi kuwa mgumu sana kwa timu zote mbili , kwanini? Uganda tayari wamesha fuzu na hawana cha kupoteza, michezo dhidi ya Tanzania , Uganda watautumia katika maandalizi na kukipima nguvu kikozi hicho. Hivyo Uganda hawata weka nguvu sana katika mchezo huo, na huenda wachezaji wake tegemeo wakaanzia sub na kutoa nafasi kwa wachezaji wengine Wa kikosi hicho, na hapo itakuwa faida kwa Tanzania kuutumia vizuri uwanja Wa nyumbani kuwafurahisha mashabiki wake.

Tanzania ndio watatangulia kufunga.
Kama wachezaji Wa Tanzania watakuwa makini kutumia nafasi watakazo pata wakati Uganda wamerilax basi tutapata Matokeo mapema.

Uganda wataamka kipindi cha pili
Uganda wataanza kuwaingiza wachezaji wake machachari kama Farouck Miya na Emanuel Okwi katika kipindi cha pili na hivyo kufanya mchezo kuwa mgumu ,

Tanzania inanafasi ya kupata goli zaidi ya mbili kipindi cha kwanza na kipindi cha pili tukawekeza nguvu kwenye idara ya kiungo cha chini na idara ya ulinzi na Uganda wakifanikiwa kuchomoa basi watachomoa goli moja hivyo mchezo kumalizika
Kwa Matokeo ya
2-1,
Ila tukipata chini ya goli mbili dakika 45, za kipindi cha kwanza basi mchezo huenda ukaenda sare ya 1-1 au 0-0
na tukizubaa wakatutangulia kwa goli 1 kipindi cha kwanza mchezo huenda ukaisha kwa Tanzania kufungwa kati ya 1-3 au 1-2.

Utabiri wangu mchezo utamalizika kwa Tanzania kushinda 2-1 all in all 90+ min ndio muamuzi.

Capeverde vs Lesotho
Katika mchezo Wa kwanza uliisha kwa Lesotho alitoa sare nyumbani dhidi ya Capeverde , mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kuliko ule Wa Uganda na Tanzania, kwanini , lethoto anaamini Uganda anaweza kupata Matokeo kwa Uganda , ya sare au ushindi na ikiwa ndivyo basi lethoto anahitaji sare tu kuingia Afcon , vile vile Capeverde anacheza nyumbani na atapambana kupata ushindi na ikiwa atapata pwenti 3 halafu Uganda apate Matokeo ya sare au ushindi basi Capeverde atakuwa amefuzu. Hivyo mchezo huu ni mgumu kwani wote wawili wana nafasi ya kusonga mbele, kutokana na ugumu Wa mchezo huo hautakuwa na magoli mengi itakuwa na chini ya magoli 2.5 yani 1-0, 0-1 au 1-1
Utabiri wangu ni Capeverde kuibuka na ushindi Wa 1-0 kulingana na uimara Wa kikosi chake all in all mpira ni 90+min


Mungu ibariki Tanzania
Atakaye pambana ndiye atashinda.

Post a Comment

0 Comments