
MWANDISHI : SALOME CLOUDY
UDSM IKS 2019
Katika mjadala huu umegawanywa katika sehemu
tatu. Sehemu ya kwanza ni utangulizi ambayo inahusu fasili ya fasihi
linganishi, sehemu ya pili ni kiini cna mwisho ni hitimisho.
Wellek na Warren (1948) wamefasili dhana ya fasihi
linganishi kuwa ni mbinu itumiwayo na wahakiki wengi wakazi ya fasihi hata
wasayansi kwakujadili njia maalumu ya usomaji wa sanaa mbalimbali ulimwenguni.
Ulinganishi unaweza kuwa wa fasihi ya Kiafrika na Kizungu ama fasili ya kizungu
dhidi ya Kihindi. Ulinganishi unahusu ulinganishaji wa kazi za mataifa
mbalimbali na sio za kitaifa peke yake.
Vilevile Henry Remark (1971) anafasili fasihi
linganishi kama uwanja wa kifasihi unao husika na uchanganuzi na mahusiano ya
kifasihi, nje ya mipaka ya nchi moja na fani nyinginezo. Mawazo ya mtaalamu
huyu hayatofautiani sana na mawazo ya wataalamu walio tangulia ingawa mtaalamu
huyu anaongeza swala la ulinganishi wa fani nyinginezo.
Kwa ujumla fasihi linganishi ni ulinganishi wa kazi
za kifasihi baina ya mwandishi mwenyewe, mwandishi na mwandishi mwingine, jamii
na jamii au taifa na taifa. Sehemu inayofuata ni jinsi historia, utamaduni na
itikadi zinavyo saidia kupambanua mawanda na mipaka katika ulinganishi wa kazi
za fasihi.
Kwanza ni historia, Historia inasaidia kulinganisha
kazi za fasihi za mtunzi mmoja au wawili zilizoandikwa katika vipindi viwili
tofauti na kuona mtagusano au mwachano wa kazi hizo kihistoria. Kwa mfano:
Katika ulinganishi wa kazi za zamani za Kezilahabi na kazi za hivi karibuni
kama kuna kufanana au kutofautiana kwa kazi hizo. Kipengele cha kihistoria
humsaidia mwanafasihi linganishi kujua kazi ya kipindi fulani cha kihistoria na
kazi nyingine ya kipindi kingine ili kutambua kama kazi hiyo hiyo imejirudia au
inautofauti. Historia huweza kumsaidia mwanafasihi linganishi kuweza kupambanua
yafuatayo,
Kujirudia kwa
Historia katika kazi za fasihi; Kwa mujibu wa Mlaga (2015), Kinacho onekana
hapa ni dhana ya umviringo au uduara. Anaendelea kusema kuwa matukio ya
kihistoria yana tabia ya kujirudia, kujirudia huko huhusisha wakati.
Mlinganishi wa kazi za fasihi kwakutumia historia anaweza kubaini ujirudiaji wa
kazi ya kifasihi katika vipindi tofauti vya kihistoria, Kwamfano tamthiliya ya Mfalme Edipode ya karne ya 5 BK
na Utenzi wa Nyakiru kibi ya
karne 19.
Mabadiliko ya
kazi za kifasihi kihistoria. Mlaga
(keshatajwa) anasema mabadiliko huweza kutokea kwa namna mbalimbali kama vile
kuhusu matukio ya zamani na athari za matukio husababisha kutokea kwa
mabadiliko. Kutokana na historia mlinganishi huweza kubaini mabadiliko ya kazi
mbalimbali kihistoria, hivyo kubaini tofauti ya kazi hizo. Kwa mfano tamthiliya
ya Kinjekitile inayohusu vita vya
majimaji kabla ya uhuru na kazi za baada
ya uhuru kama vile Miradi bubu ya wazalendo. Kwakumakinikia historia mwanafasihi
mlinganishi huweza kubaini mabadiliko katika kazi hizo.
Pili, Utamaduni; Ni jinsi binadamu anavyo kabili
maisha katika mazingira yake, ambapo hujumuisha ujuzi, imani, Sanaa, maadili,
sheria mila na desturi. Katika kipengele hiki mlinganishaji wa kazi ya fasihi humakinikia
kuangalia vielelezo vya kitamaduni katika kazi hizo na kuvilinganisha ambapo
huweza kubaini na kupambabua mambo
yafuatayo;
Kuingiliana kwa vipengele vya kitamaduni; Katika kumakinikia Utamaduni mlinganishaji
huweza kubaini kuingiliana kwa baadhi ya vipengele vya kitamaduni katika kazi
mbili za kifasihi za jamii tofauti. Kwa mfano: Mlinganishaji anapolinganisha
tamthiliya ya Lina Ubani na
tamthiliya na Kwenye Ukingo wa Thim atakuta
kuna kufanana kwa kipingele cha Utamaduni kuhusu swala la ndoa, ambapo kwao
kuoa kabila kingine ni kosa.
Kutofautiana kwa baadhi ya vipengele vya kitamaduni;
Mlinganishaji wa kazi ya fasihi anapo jikita katika kulinganisha kazi za
kifasihi kitamaduni anaweza kubaini kutofautiana kwa vipengele vya kitamaduni
baina ya jamii na jamii. Kwa mfano: Wimbo wa Lawino kilicho tafsiriwa na
Paul Sozigwa.
Kipengele kingine ni itikadi. McClosky (1964) anaeleza kuwa itikadi ni
mfumo wa imani ambao unaeleza, kujumuisha na kufafanua masuala ya madaraka,
haki za binadamu na kutathimini masuala ya kihistoria ili kufanya maamuzi
sahihi kwa wakati uliopo na ujao. Itikadi katika jamii ndiyo inaeleza namna
viongozi, haki za binadamu, masuala ya dini namna vinavyomuongoza binadamu
katika maisha. Itikadi inamsaidia mlinganishi wa kazi za fasihi kujua imani ya
mwandishi mmoja katika kazi zake au kazi za waandishi wawili tofauti. Katika
kumakinikia itikadi katika ulinganishaji wa kazi za kifasihi mwandishi huweza
kubaini,
Kufanana kiitikadi baina ya kazi tofauti za
mwandishi mmoja; Katika ulinganishaji wa kazi za kifasihi kwa kjtumia kipengele
hiki cha itikadi mlinganishi huweza
kubaini ufanano wa itikadi katika kazi za msanii mmoja kwa mfano Chuachua
(2011) ameeleza kuhusu itikadi katika riwaya za Shaaban Robert kama
vile Kusadikika na Kufikirika ambazo itikadi ya umoja na
ushirikiano imejitokeza.
Kutofautiana kwa itikadi baina ya kazi ya mwandishi
mmoja na mwingine; Katika kuangalia
kipengele cha kiitikadi katika kazi za kifasihi ulinganishaji huweza kupambanua
tofauti baina ya kazi hizo kwa mfano
kutofautiana kwa itikadi baina ya kazi za Emanuel Mbogo na kazi za Penina Mlama
kuhusu itikadi zao juu ya mwanamke.
Kwa ujumla katika kulinganisha mawanda ya kazi za
fasihi mlinganishaji ataangalia itikadi, historia na utamaduni. Huku akijikita
katika nadharia mbalimbali za fasihi kama vile katika historia mlinganishi
atatumia nadharia ya U-historia, katika Utamaduni anaweza kutumia Ufeministi na
katika itikadi anaweza kutumia nadharia ya Ubaada ukoloni.
MAREJELEO
Chuachua, R. (2011), ItikadikatikaRiwayazaShaaban Robert. TATAKI: Dar es salaam.
McClosky, F (1964), Consensus and Ideology in American Political Science Review 58
(June)
361-82.
Mlaga, W. (2005), UhistoriakatikaRiwayaya Kiswahili: Mifanokutokariwayaza ‘Ndotoya
Ndaria’‘Gamba
la Nyoka’ na ‘MiradiBubuyaWazalendo’. University of
Rwanda:
Rwanda.
Remark, H.H. (1971), ComperativeLiterature: its definition and Function. Southern
illios:
Wellek, R. na Warren, A. (1948), Theory of Literature. Harcourt, Brace
and Company:
New York.
0 Comments