Hyman
(1975) anafasili dhana ya Fonetiki kuwa ni taaluma ambayo huchunguza sauti
ambazo hutumiwa na wanadamu wakati wanapowasiliana kwa kutumia lugha.
Pia
Massamba na wenzake (2004) wanafasili Fonetiki ni tawi ambalo hujishughulisha
na uchambuzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usikikaji na
ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla.
Vile
vile Matinde (2012) anafasili kuwa neno “Fonetiki” limetokana na neno la
Kigiriki “Phonetic” ambalo limeundwa na maneno mawili “Phone” (sauti) na “tic” (uchunguzi). Hivyo,
anafasili dhana ya Fonetiki kuwa ni taaluma ya isimu inayochunguza foni (sauti
zote zinazotamkwa na binadamu ambazo hazihusishwi na lugha maalumu au
mahususi).
Mgullu
(1999:30) anafasili Sifa bainifu ni sifa ambazo hutumiwa kuzibainisha foni.
Kila foni inaweza kupambanuliwa kwa kutumia sifa maalumu za foni fulani na
jumla ya sifa hizo, ndizo ambazo huipambanua foni hiyo na pia huitofautisha na
foni nyingine.
Pia
Massamba na wenzake (2004:80) anafasili Sifa bainifu kuwa ni nduni zitumikazo
kutofautisha kipashio kimoja na kipashio kingine cha aina yake.
Hivyo,
Sifa bainifu ni nduni zitumikazo kubainisha foni moja kuwa au kutokuwa na sifa
fulani tofauti na nyingine.
Katika
lugha ya Kiswahili, sauti zimegawanyika katika makundi makuu mawili yaani sauti
za konsonati na sauti za irabu. Mgullu (1999) anafasili Irabu ni sauti
zinazotamkwa bila ya kuwa na kizuizi chochote katika mkondo hewa. Kwa mujibu wa
Daniel Jones kama alivyonukuliwa na Mgullu (keshatajwa) anasema irabu msingi za
Kiswahili ambazo hazihusishwi na lugha yoyote ni nane tu. Irabu hizo ni [a], [e],
[i], [o], [u], [а], [ε], [ͻ]. Vilevile kwa upande wa konsonanti, Mgullu
(keshatajwa) anafasili kuwa ni sauti zinazotamkwa kwa kuwepo na kizuizi katika
mkondo hewa. Katika lugha ya Kiswahili kuna jumla ya konsonanti ishirini na
sita (G26) ambazo ni; [b], [d],
[f], [g], ch [tʃ], dh [ð], gh [ɤ], [h], j [Ɉ], [k], kh [x], [l], [m], [n], ng’
[ŋ], ny [ր], [p], [r], [s], sh [ʃ], [t], th [Ө], [v], [w], y [j] na [z].
Zifuatazo
ni sifa bainifu za kifonetiki za irabu za Kiswahili kama zilivyobainishwa na
Mgullu (1999), ambapo amezingatia sifa kuu tatu yaani mahali pa kutamkia irabu,
mwinuko wa ulimi na mkao wa mdomo.
Sifa
ya mahali pa kutamkia irabu, kuna sehemu kuu tatu ambazo hutumika kutofautisha
irabu. Sehemu hizo ni sehemu ya mbele ya ulimi, sehemu ya kati ya ulimi na
sehemu ya nyuma ya ulimi. Sifa ya mwinuko wa ulimi, wanafonetiki wamegundua ya
kuwa mwinuko wa ulimi ni wa aina nne;
mwinuko wa chini, mwinuko wa nusu – chini, mwinuko wa nusu – juu na mwinuko wa
juu. Sifa ya mwisho ni mkao wa mdomo, ambapo wanafonetiki wameafikiana ya kuwa
wakati wa kuzitamka irabu midomo huweza kukaa kwa namna kuu mbili yaani mkao wa
mviringo na mkao wa mtandazo. Mathalani katika kielelezo kifuatacho
kinadhihirisha sifa hizo;-
Hivyo,
irabu msingi zinaweza kupambanuliwa kwa kutumia sifa bainifu tulizozijadili
hapo juu kama ifuatavyo;-
[i] [u] [e] [o] [a]
+
irabu + irabu + irabu +irabu+ irabu
+
mbele + nyuma + mbele + nyuma+ nyuma
+
juu + juu + nusu juu
+ nusu chini + chini
+
mtandazo + mviringo + mtandazo + mviringo + mviringo
[ε] [ͻ] [а]
+
irabu + irabu + irabu
+
mbele + nyuma + mbele
+
nusu juu + nusu chini + chini
+
mtandazo + mviringo + mtandazo
Baada
ya kubainisha sifa pambanuzi za irabu; zifuatazo ni sifa bainifu za kifonetiki
za konsonanti zote za sauti za Kiswahili.
Ubainishaji
wa sifa za konsonanti hutofautiana kutoka mtaalamu mmoja na mwingine. Mfano
Jakobson na Halle miaka ya (1950), kama walivyonukuliwa na Mgullu (1999)
walizipambanua konsonanti kwa kutumia sifa za kiakustika. Wao walikuwa na
makundi matatu ya sifa ambayo ni sifa ya usonoranti, sifa ya uprotensi na sifa
ya utoni. Baadaye Morris Halle alishirikiana na Noam Chomsky kuzipitia tena
sifa za Jakobson na Halle na wakazigawa upya katika makundi makuu matano.
Makundi hayo ni sifa za makundi makuu, sifa za chemba, namna ya kutamka, sifa
chasili na sifa za kiarudhi. Lakini inaonekana kuwa sifa hizo zilizobainishwa
na wanaisimu hao wakongwe, zilibuniwa ili kukidhi mahitaji ya kupambanua
konsonanti zilizoonekana katika lugha ya Kihindi- Kizungu. Hivyo kama sifa
fulani haisaidii kubainisha kitamkwa chochote katika lugha fulani, basi hiyo si
sifa bainifu katika lugha hiyo na haina maana yoyote kuitumia.
Kwa
mantiki hiyo, ingawa sifa bainifu tulizojadili hapo juu ni nyingi, lakini sifa
zinazotakiwa kutumiwa wakati wa kuzibainisha konsonanti za lugha fulani
mahususi, si lazima ziwe nyingi. Mathalani katika lugha ya Kiswahili,
konsonanti zinaweza kubainishwa kwa kutumia sifa bainifu tano tu ambazo ni
ukonsonanti, namna ya kutamka, mahali pa kutamkia, mkao wa glota na unazali.
(Mgullu (1999).
Sifa
ya ukonsonanti, konsonanti zote zinabainishwa kuwa na sifa hiyo yaani [+
konsonanti]
Sifa
ya namna ya kutamka, inatusaidia kubainisha vitamkwa katika yale makundi
makubwa kama vile; vipasuo (vizuiwa), vikwamizi, vizuiwa- kwamizi, vitambaza,
vimadende, nazali na nusu- irabu (viyeyusho).
Vipasuo
(vizuiwa), ni sauti ambazo zinapotamkwa hewa hutoka mapafuni, husukumwa nje na
kuzuiwa kabisa kabla ya kuachiliwa kwa gafla na kutoa sauti ambayo hufanana na
sauti za mlipuko. Vipasuo hivyo katika Kiswahili ni [p], [b], [t], [d], [k] na
[g].
Vikwamizwa,
ni sauti zinazotamkwa wakati ambapo, ala za kutamkia zinapokuwa zimekaribiana
kiasi cha kutosha kuweza kusikika mkwaruzo unaotokea wakati hewa inapopita kati
ya ala hizo. Vikwamizwa vilivyopo katika lugha ya Kiswahili ni [v],[f], [h],
[z], [x], [s], [Ө], [ɤ], [ð] na [ʃ]
Vizuiwa-
kwamizwi, ni konsonanti ambazo wakati wa kutamka hewa husukumwa nje kwa nguvu,
huzuiwa halafu nafasi ndogo huachiwa ili hewa ipite ikiwa na mkwaruzo. Mfano
konsonanti hizo ni [tʃ] na [Ɉ]
Vitambaza,
ni konsonanti ambazo hutamkwa kwa hewa kusukumwa nje, kuzuiwa na kuruhusiwa
kupita pembeni mwa kizuizibila kwaruzo mkubwa sana. Mfano wa kitambaza ni
konsonanti [l].
Vimadende,
hutamkwa huku ncha ya ulimi ikiwa imeugusa ufizi lakini kutokana na nguvu ya
hewa inayopita katikati ya ncha hiyo na ufizi, ncha ya ulimi hupigapiga haraka
haraka kwenye ufizi. Kwenye Kiswahili kuna kimadende kimoja ambacho ni [r].
Nazali,
ni aina ya konsonanti ambazo hutamkwa kwa namna ya kukishusha chini kinywa kwa
namna ambayo kiasi kikubwa cha hewa kutoka mapafuni huelekea kupitia kwenye
chemba cha pua. Kiswahili kina nazali zipatazo nne ambazo ni [n], [m], [Å‹] na[Ö€].
Sifa
ya mahali pa kutamkia, hutusaidia kuonyesha mahali ambapo kila sauti hutamkiwa.
Mfano kuna sehemu mbalimbali za kutamkia kama vile; midomo, ufizi, kaakaa
laini, kaakaa gumu, glota, chemba cha pua na meno.
Sifa
ya glota, inatusaidia kutofautisha kati ya zile sauti ambazo ni ghuna na zile
ambazo si ghuna. Mathalani foni [p] na [b] zinafanana kwa sifa zingine zote,
isipokuwa hutofautiana katika sifa ya mkao wa glota. Foni [p] ni sighuna
[-ghuna] lakini foni [b] ni ghuna [+ghuna].
Sifa
ya mwisho ni Unazali, ambapo hutusaidia kubainisha zile foni ambazo zina sifa
ya unazali [+unazali] na zile foni zingine ambazo hazina sifa ya unazali yaani
[-unazali]
Ufuatao
ni ufafanuzi unaobainisha sifa za kifonetiki za sauti za konsonanti za
Kiswahili.
Vizuiwa/
vipasuo
[p] [b] [d] [t] [k] [g]
+
kons + kons + kons + kons + kons + kons
+
kipasuo + kipasuo + kipasuo +
kipasuo + kipasuo + kipasuo
+
a mdomo + a mdomo + ufizi + ufizi + kk laini + kk laini
-
unazali- unazali - unazali - unazali - unazali - unazali
-
ghuna+ ghuna + ghuna - ghuna
- ghuna + ghuna
Vikwamizwa
[f] [v] [Ө] [ð] [s]
+
kons + kons + kons + kons + kons
+
kikwamizwa + kikwamizwa + kikwamizwa + kikwamizwa + kikwamizwa
+
a mdomomeno + a mdomomeno+ meno + meno + ufizi
-
unazali - unazali - unazali - unazali - unazali
-
ghuna + ghuna - ghuna + ghuna - ghuna
[z] [x] [ɤ] [ʃ] [h]
+
kons + kons + kons +
kons + kons
+
kikwamizwa+ kikwamizwa+ kikwamizwa + kikwamizwa + kinusa
+
ufizi+ kk laini + kk laini+
kk –a ufizi + glota
-
nazali - unazali - nazali - nazali- nazali
+
ghuna - ghuna+
ghuna - ghuna - ghuna
Vizuiwa
kwamizwaKitambaza
Kimadende
[tʃ][Ɉ] [l] [r]
+
kons+ kons +
kons + kons
+
kizukwa + kizukwa + kitambaza + kimadende
+
kk gumu+ kk gumu + ufizi + ufizi
-
unazali- unazali - unazali - unazali
-
ghuna+ ghuna + ghuna + ghuna
Nusu
irabu
[w] [j]
+
nusu irabu + nusu
irabu
+
midomo/ kk laini + kk gumu
-
Unazali - unazali
+
ghuna + ghuna
Nazali
[m] [n] [Ö€] [Å‹]
+
kons + kons + kons + kons
+
nazali + nazali + nazali + nazali
+
midomo + ufizi + kk gumu+ kk laini
+
unazali + unazali + unazali + unazali
+
ghuna + ghuna+ ghuna + ghuna
Kwa
ujumla fonetiki imetoa mchango mkubwa sana katika kuzitambua sauti na sifa zake
kwa ujumla katika lugha nyingine na katika lugha ya Kiswahili. Ambapo katika
lugha ya Kiswahili imetusaidia kubainisha utofauti uliopo katika kuzipambanua
sifa za konsonanti na irabu na katika vipashio vya aina yake.
MAREJELEO
Hyman,
L. M. (1975). Phonology: Theory and Analysis. New York: Holt, Rinehart &
Winston.
Massamba,
D. P. B. na wenzake .(2004). Sarufi
Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo
(SAMIKISA).
Dar es salaam: TUKI.
Matinde,
R. S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati
na
Vyuo Vikuu. Tanzania- Mwanza: Serengeti
Educational Publishers Ltd.
Mgullu,
R. S. (1999). Mtalaa wa Isimu. Uganda
– Kampala: Longhorn Publishers (U) Ltd.

0 Comments