WANAFUNZI watatu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Makurugusi, wilayani Chato Mkoa wa Geita wamepoteza maisha baada ya mtumbwi waliokuwa wakiutumia kufanya utalii Ziwa Victoria kuzama.
Tukio la kuzama kwa wanafunzi hao limetokea jana Jumanne Juni 4, 2019 saa tano asubuhi wakati wanafunzi hao wakifanya utalii wa ndani katika eneo la ufukwe wa Ziwa Victoria katika mwalo uliopo Makurugusi.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo la mtumbwi waliokuwa wakitumia akisema wanafunzi hao walikua watano watatu wamepoteza maisha, wawili waliokolewa na mmoja hali yake ni mbaya ambaye amelazwa hospitali ya wilaya ya Chato.
Amesema miili ilipatikana jana saa 11 jioni na imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato wakati taratibu za mazishi zikiendelea.

0 Comments