O-rejeshi ni kiangama au umbo linalopachikwa kwenye kitenzi ili kuonesha urejeshi katika nomino. Huweza kujitokeza katikati mwa kitenzi au mwishoni.
Mfano Wa viambishi vya O-rejeshi
-ye-
-o-
-yo-
-lo-
-cho-
-vyo-
-zo-
-ko-
-po-
-mo-
mifano katika sentensi/vitenzi.
1. Ali vyo mpiga
2. Kili cho potea.
Masharti ya upachikaji wa O-rejeshi
a) nilazima pawepo na upatanisho wa kisarufi na nomino inayorejelewa.
mfano
chakula ki- li-cho-pikwa hakiliki
-ki- inapatana kisarufi na -cho-
b. Katika ngeli ya kwanza umoja, yani a/wa , kiangama -o- hubadilika na kuwa -e-
Kwamfano
Mtoto ali-ye- potea amepatikana
dhima ya O-rejeshi
1. Kuonesha mtenda au mtendwa wa jambo
2. Kuonesha upatanisho wa kisarufi
3. Huweza kubainisha umoja na wingi
4. Hudokeza njeo
5. Hudokeza namna
www.masshele.blogspot.com
0 Comments