Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MCHANGO WA TEHAMA KATIKA UTOAJI WA KITABU







E.masshele 2019

1.0 Utangulizi
Sehemu hii tumefasili dhana mbalimbali zinazohusiana na swali hili lakini pia tumeeleza kwa ufupi historia nas maendeleo ya TEHAMA.
TUKI (2014) wanafalisi kitabu ni kurasa zenye maandishi zilizofungwa pamoja kwa utaratibu maalumu. Udhaifu wa fasili hii ni kwamba imegemezwa kwenye nakala ngumu ilhali vipo vitabu vilivyo katika nakala laini.
Wamitila (2016) Kitabu ni maandishi yaliyowekwa pamoja katika kurasa zilizoandikwa kwa mkono au zilizopigwa chapa na kupangwa kwa utaratibu maalumu na kuitwa jalada. Fasili hii haitofautiani sana na ile ya TUKI (2014) kwakuwa imeegemezwa sana kwenye nakala ngumu.
Kwa ujumla, kitabu ni  muunganiko wa vipande vya karatasi au kurasa zilizo katika nakala laini zilizoandikwa au kuchapwa na kuweka pamoja katika jalada.
Kwa mujibu wa Collins (2019) TEHAMA ni shughuli au mchakato unaohusisha kompyuta na vifaa vingine vya teknolojia umeme. TEHAMA ni kifupisho cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Lawson (2006) anaeleza kuwa TEHAMA katika uchapishaji wa vitabu ilishika kasi katika karne ya 19 ambapo anayataja makampuni kadhaa yaliyotumia TEHAMA kwa kiwango cha juu katika utoaji wa kitabu kama vile Macmillan, Oxford University, Cambridge University Press, Penguin Group UK, Random House Group na Blackwell Publishers. Hii ilikuwa ni hatua kubwa katika tasnia ya uchapishaji kama asemavyo Chan (2000) TEHAMA ilibadili namna ya ufanyaji kazi, kwa mfano kuanza kutumika kwa word processor kulisababisha uandikaji wa haraka wa maandishi. Vilevile, Lawson (2006) akimrejelea Awang (2003) anasema kuwa matumizi ya TEHAMA yalichochea kuendelea kwa tasnia ya uchapishaji katika miaka ya 1980. Balkwill (1999) anasema kuwa TEHAMA ilisababisha uchapishaji kuonekana rahisi na kuruhusu uchapishaji binafsi.
2.0  Kiini
Katika sehemu hii tutajadili mchango wa TEHAMA katika hatua zote muhimu za utoaji wa kitabu, mchango huo ni kama ufuatao:


2.1  Uandikaji wa mswada
Uandikaji wa mswada ni hatua ya mwanzo ya mchakato wa utoaji wa kitabu ambapo mwandishi ndiye mwenye jukumu la kubuni wazo au kisa, kukifanyia utafiti unaohitajika na kugeuza wazo hilo kuwa mswada. Katika hatua hii TEHAMA inamchango ufuatao:
2.1.1 Mwandishi huweza kutumia programu mbalimbali na vifaa vya KITEHAMA katika  uandishi wa mswada.
Vifaa hivyo ni kama vile kompyuta, ambapo Chan (2000) anasema kuwa TEHAMA ilibadili namna ya ufanyaji kazi, kwa mfano kuanza kutumika kwa word processor kulisababisha uandikaji wa haraka wa maandishi. Hivyo, kwa kutumia kompyuta husaidia uandishi wa haraka wa mswada na uhariri wa awali, hii humsaidia mwandishi kupunguza gharama.
2.1.2 Kwa kutumia program mbalimbali za  intaneti kama vile Google
Mwandishi huweza kutafuta kampuni bora ya kuchapishia mswada wake. Kwakutumia program tumishi za kimtandao mwandishi huweza kutafuta taarifa kuhusu kampuni mbalimbali za uchapishaji na kunga’amua ni kampuni ipi bora ya kuchapishia mswada wake.
2.1.3 Kwa kupitia TEHAMA mwandishi  anaweza kuwasiliana na kutuma mswada wake kwa kutumia barua pepe
Ambapo huweza kuwasiliana na mhariri kuhusiana na mswada wake. Aidha kwakupitia TEHAMA mwandishi huweza kuhifadhi mswada wake kwa kutumia Google Cloudy, na Clouds sever na kuufanya kuwa salama bila kupotea.
2.2  Uhariri
Mulokozi (2014) anaeleza kuwa ni mchakato wa kugundua, kuteua, kutafuta na kuandaa mswada kwa ajili ya uchapishaji ili uweze kwenda kwa msanifu. Katika hatua hii pia TEHAMA imekuwa na mchango mkubwa kwan huwezai humsaidia mhariri kama ifuatavyo;


2.2.1 Kwa kutumia kompyuta husaidia kupunguza gharama.
Mathalani, Lawson (2006) anasema kuwa teknolojia ya kidijitali ilisababisha kuongezeka kwa uzalishaji na kupunguza gharama katika kushughulikia mswada, kuseti na kusoma prufu. Hivyo TEHAMA, inao mchango mkubwa katika kukamilisha mchakato wa uhariri kwa urahisi.
 2.2.2 Kupitia mifumo ya KITEHAMA, mhariri huweza kuwasiliana na mwandishi wa mswada kwa haraka.
Hii inamaana kuwa katika, mchakato wa uhariri, mhariri huweza kupokea mswada kutoka kwa mwandishi kupitia barua pepe, na kufanya mawasiliano na mwandishi kwa kutumia vifaa mbalimbali vya TEHAMA, kamavile kompyuta na simu za kisasa.
2.3 Kusanifu
Huu ni upangaji wa kurasa za kitabu, mtandazo wa maandishi na michoro katika kurasa na uunganishaji wa kurasa hizo katika umbo au ukubwa fulani. TEHAMA ina nafasi/mchango ufuatao katika hatua hii ya utoaji wa kitabu.
2.3.1 Hurahisisha mchakato wa usanifu wa kitabu
Mathalani, Ihebuzor (2016) anaeleza kuwa shughuli ya usanifu kwa sasa hufanyika haraka na kwa urahisi kutokana na maendeleo ya TEHAMA tofauti na ilivyokuwa awali. Hii ina maana kuwa usanifu hutumia program mbalimbali za kompyuta kamavile za kuchora, kupanga kurasa hata suala la rangi ya maandishi.
2.4  Uchapaji
Kwa mujibu wa Mulokozi (2014) katika hatua hii anaeleza kuwa mchapaji ndiye mpiga chapa wa kitabu. Yeye huwa na matbaa na kutoa nakala nyingi za kitabu kulingana na maagizo ya mchapishaji. Aidha, katika hatua hii TEHAMA imekuwa na mchango mkubwa kama ufuatao:
2.4.1 Husaidia katika uchapaji wa kidigitali
Kwa mujibu wa Olsen na wenzake (2015) wanaeleza kuwa kupitia uchapishaji wa kidigitali huweza kuwa na uchapaji binafsi ambapo mtu anaweza kuchapa kwa kutumia kompyuta iliyounganishwa na mashine ndogo ya kupigia chapa.
2.5 Uuzaji na usambazaji
Hii ni hatua ya mwisho ambapo kitabu huwekwa sokoni ili kimfikie msomaji na kuifaidisha kampuni iliyohusika katika mchakato mzima wa uchapishaji. Aidha, TEHAMA ina nafasi kubwa katika uuzaji na usambazaji wa kisasa, ufuatao ni mchango wake:
2.5.1 Hurahisisha usambazaji na uuzaji wa haraka wa vitabu kwa njia ya mtandao
Okwilagwe (2017) wanaeleza kuwa TEHAMA imeleta mapinduzi makubwa sana katika suala la uuzaji na usambazaji wa vitabu. Anaendelea kueleza kuwa hii ni njia bora ya uuzaji na ufikiaji wa wateja kwa haraka tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo mteja alipaswa kwenda dukani kupata nakala ya kitabu anachokihitaji. Lakini kwa kutumia mtandao mteja huweza kupata kitabu kilichopo katika nakala laini kwa kupitia maduka ya mtandao kama vile Amazon, E-bay na Lulu.com. Pia katika hatua hii TEHAMA ina mchango ufuatao:
2.5.2 Husaidia katika kukitangaza kitabu
Kupitia media mbalimbali kama vile redio, televisheni, baruapepe, na matangazo ya mtandaoni,  media hizi muuzaji wa kitabu huweza kukitangaza kitabu hicho na kikatambulika na wengi kutokana na idadi kubwa kutumia vifaa vya kidigitali kama vile simu hata kompyuta . Hivyo, kupitia matangazo hayo humsaidia muuzaji kupata wateja wengi wa ndani na nje ya nchi.
3.0 Hitimisho
Kwa ujumla, licha ya TEHAMA kuwa na mchango mkubwa katika hatua za utoaji wa kitabu vilevile matumizi ya TEHAMA hususani kwa nchi zinazoendelea zinakumbwa na changamoto mbalimbali kama vile maendeleo duni ya kiteknolojia na umasikini.s





MAREJELEO
Balkwill, R. (1999). Supporting Creativity in the Supply Chain: The Role of  Creative Terms in The Authoring Process, Publishing Research Quartely, 15(30 – 46)
Chan, Stephen, L. (2000). Information Technology in Business Process Management. Journal, 6 (3), 224 -237)
Collins (2019). Advanced English Dictionary. London: Collins Publishers.
Lawson, A. (2006). The Effect of ICT on the UK Book Publishing Industry. UK: University of Manchester.
Okwilagwe, O. A. (2017). Information and Communication Technology Use in Book marketing by Emerging Indigenous Publishing Firms and Booksellers in Ibadan Metropolis. Ibadan: University of Ibadan.
Olsen, K. (2016). Report to NGU  on Digital Print.
TUKI (2014). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam. Oxford University Press.
Wamitila, K. W. (2016). Kamusi Pevu ya Kiswahili. Nairobi: Vide-Muwa.
www.masshele.blogspot.com



Post a Comment

0 Comments