CHUO KIKUU CHA KENYATTA
IDARA YA KISWAHILI
WAMALWA STEPHEN
MATINI YA AKS 300 — MOFOLOJIA NA SINTAKSIA
SEPTEMBA — DESEMBA 2016/2017
Mbinu za kuunda misamiati na Istilahi
Ukopaji
Kukopa ni mbinu inayotumiwa na lugha zote za ulimwengu kurutubisha msamiati wake.
Kiswahili huunda msamiati, maneno na istilahi mpya kupitia mbinu ya kuazima maneno kutoka kwa lugha zingine.
Kiswahili kimeazima maneno kutoka kwa lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kihindi, Kireno, Kituruki, Kishirazi, na Kijerumani na hata lugha za Kiafrika.
Lugha asili Maneno yaliyokopwa
Kishirazi mnara, nanga, kiwida
Kihindi pesa, bima, laki, godoro
Kituruki baruti, bahasha, korokoroni
Kireno karata, pera, bendera, mvinyo
Kijerumani hela, barawani, shule
Kiingereza Mei, daktari, kampuni, eropleni
Kiarabu Rehema, faraja, alhamisi
Kinyamwezi ikulu, kabwela, bunge
Kikuyu matatu, githeri
Kipare kitivo
Kimasai mbuti, ngalemu
Sababu za kukopa maneno
Huenda neno linalokopwa linasimamia kitu ambacho hakipo katika utamaduni kopaji.
Kasumba ya uzungumzaji hivi kwamba wazungumzaji hupendelea kutumia maneno fulani kuliko mengine.
Maingiliano marefu ya kitamaduni na kijamii.
Utabaka: Lugha inayohisiwa kuwa ni ya tabaka la chini hukopa kutoka kwa lugha ya tabaka la chini.
Aina za Ukopaji
Kukopa kwa Tafsiri
Tafsiri ni uhawilishaji (uhamishaji) wa mawazo, ujumbe, au taarifa iliyopo katika maandishi kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa bila kupoteza maana ya msingi na mtindo uliotumika katika matini chanzi
Tafsiri huzingatia muundo wa lugha pokezi.
Katika mbinu hii vifungu katika lugha asilia hutafsiriwa katika lugha kopaji.
Kiswahili kimetumia mbinu hii kujenga msamiati na istilahi zake.
Kwa mfano
Kiingereza
Kiswahili
Free market
Soko huria
Ruling party
Chama tawala
Opposition party
Chama cha upinzani
Commissioner General
Kamishena mkuu
Electoral Commission
Tume ya Uchaguzi
Ubora wa mbinu hii.
Mbinu hii huzingatia kigezo cha maana zaidi kuliko muundo wa maneno yaliyochukuliwa toka lugha chanzi na kutafsiriwa ili kuafiki utamaduni wa lugha lengwa.
Hali hii husaidia katika kuunda maneno yenye maana iliyo wazi na inayokubalika katika lugha lengwa.
Udhaifu wa mbinu hii.
Mara nyingi huwa vigumu kutafsiri baadhi ya maneno kutoka lugha chanzi kwa kufuata kigezo maana.
Kuna uwezekano wa kupata tafsiri ambazo hazina maana wala mantiki katika lugha lengwa.
Mfano; Kitchen Party - sherehe ya jikoni.
Things fall Apart - vitu vilivyoanguka na kutapakaa.
Mobile phone - simu za kurandaranda (simu za mikono)
Sick leave - likizo ya ugonjwa
Dictatorship - uongozi wa imla (uongozi wa kimabavu yafaa zaidi)
Kukopa kwa utohozi
Kupitia kwa mbinu hii wanalugha wanachukua maneno kutoka kwa lugha asilia na kunukuu kwa kuangalia fonolojia ya lugha pokezi.
Neno linatamkika kwa utaratibu wa lugha pokezi.
Maneno yaliyotoholewa hupata maana kutokana na lugha kwa kufuata kaida au sheria za kifonolojia na kimofolojia za lugha pokezi kabla ya kutumiwa.
Neno linapotoholewa hutamkwa na kuandikwa kwa utaratibu wa lugha pokezi.
Hata hivyo maana ya neno lililotoholewa hubakia ileile ya awali.
Kiingereza
Kiswahili
Switch
Swichi
Lorry
Lori
Budget
Bajeti
Agenda
Ajenda
Biology
Baolojia
Dollar
Dola
Oxygen
Oksijeni
Ubora wa mbinu hii:
Mbinu hii ya utohozi ni mbinu rahisi ya kutumiwa katika uundaji wa msamiati. Mzungumzaji yeyote anaweza kutumia mbinu hii hata bila kuhudhuria kozi yoyote ya isimu au kufundishwa.
Maneno mengi huweza kuundwa kwa kutumia mbinu hii ili kukidhi mahitaji ya matumizi katika lugha mbalimbali.
Udhaifu wa mbinu hii.
Mbinu hii hulemaza ubunifu wa wanajamii katika kuunda msamiati mpya wenye kuakisi utamaduni wa jamii husika.
Lugha ya utohozi huonekana kukosa uasilia yaani lugha huonekana kuwa chotara.
Baadhi ya maneno katika Kiswahili ambayo yametoholewa kutoka lugha ya kiingereza katika lugha ya Kiswahili hutamkwa kwa namna tofauti kabisa.
Tazama:
Kiingereza
Kiswahili
Data
Deta
Dance
Densi
Bank
Benki
Radio
Redio
Kukopa sisisi
Huu ni ukopaji wa moja kwa moja.
Hapa maneno yanachukuliwa yalivyo katika lugha chasili na kutumiwa katika lugha kopaji.
Neno Lugha Chasili
Kitivo Kipare
Ikulu Kinyamwezi
Githeri Kikuyu
Nyuni Luhya
Mwambatano
Mbinu hii inahusu kule kuunganishwa kwa maneno mawili kuzua neno moja lenye maana mpya tofauti na maneno yaliyoiunda.
Yaweza kuwa:
Nomino Nomino - Mwana +jeshi=mwanajeshi, duara+dufu=duaradufu, batamzinga
Nomino Kivumishi — Ngombe+jike=ngombejike, mja + mzito=mjamzito, pembe + nne=pembenne, chungu + -zima=chungunzima
Nomino Kitenzi — Nukta+tulia = nuktatulia
Kitenzi Nomino - pima + mvua kipimamvua, changa + moto changamoto, chemsha + bongo =chemshabongo ,fungua + kinywa kifunguakinywa
Kitenzi Kielezi - ona + mbali kionambali
Udhaifu wa mbinu hii
Maneno mawili yenye maana tofauti huambatanishwa pamoja kuzua neno moja, jambo ambalo lina uzito wa kisemantiki.
Huyahitaji maneno kutumika mpaka yazoeleke.
Unyambuaji
Maneno yanaweza kunyambuliwa kwa kuongeza au kupachika viambishi awali na tamati ili kupata maneno tofauti.
Katika mbinu hii viambishi vinaongezwa katika mizizi mwafaka kuzua neno jipya.
Aina tofauti za unyambuaji
Unyambuaji kwa kutumia viambishi.
Hapa maana mpya la neno hupanuka kupitia viambishi.
Kwa mfano Kutokana na mzizi —pik- tutapata pikia, pikiwa, pikika, mpishi.
Unyambuaji wa viambishi nomino
Huundwa kutokana na vitenzi.
Kitenzi nomino
tafiti utafiti
chuma uchumi
soma Msomi
Ufupishaji
Ni mbinu ya kuunda maneno kwa kutumia vifupisho.
Kuna mbinu kadhaa zinazotumika katika kufupisha maneno ukapata mengine mapya.
Ufupishaji mkato
Katika mbinu hii, neno hufupishwa kabisa na vifungu vichache hutumika.
Baadhi ya vipashio au silabi hudondoshwa na kuacha tu sehemu ya neno asilia.
Mifano.
Baba — Ba
Dar es Salaam — Dar
Bibi — Bi.
Mama - Ma
Akronimu
Kutumia silabi za mwanzo za maneno fulani katika kirai kuunda neno.
Mifano UKIMWI - Ukosefu wa Kinga Mwilini.
TUKI - Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
Uhulutishaji.
Ni mbinu ambayo hutumika kwa kufupisha virai ili kupata maneno.
Mara nyingi sehemu ya mwanzo ya kirai cha kwanza huunganishwa na sehemu ya kwanza ya neno la pili kuunda neno jipya.
Vijisehemu hivi vya maneno huwekwa pamoja kuunda neno jipya.
Mfano
Chakula cha jioni - Chajio.
Chakula cha mchana - Chamcha
Mtu asiye na kwao - Msikwao
Kubuni
Ubunifu ni mbinu ya kuunda msamiati katika lugha husika na hurejelea dhana au vitu vipya ambavyo hapo awali havikuwepo katika jamii husika.
Ni mbinu ambayo hutumiwa badala ya kuchukua maneno kutoka lugha nyingine.
Njia mbalimbali za kuunda msamiati kwa njia ya kubuni.
kubuni kwa kinasibu
kubuni kwa kuongozwa na vigezo maalumu.
Kubuni kwa kinasibu
Huku ni kuzipanga fonimu za lugha kulingana na utaratibu wa ujenzi wa lugha inayohusika iili kuunda neno ambalo halipo katika lugha.
Kwa njia hii, maneno mapya ya lugha huundwa kwa kuzingatia kanuni za isimu za lugha husika.
Njia hii hutatua tatizo la kuchukua maneno ambayo tayari yapo katika lugha zingine.
ndege - kisopo
Macho - Maninga —
kubuni kwa kuongozwa na vigezo maalumu
Mbinu hii huweza kudhihirishwa kwa njia mbalimbali;
Uakisi wa umbo la kirejelewa.
Kuna leksia za Kiswahili ambazo huakisi umbo la kiashiriwa.
Kwa mfano; .
Neno ̔ Nyoka huibua taswira ya kitu kilichonyooka.
Neno pembe kali hurejerea umbo lenye pembe.
Neno kidole tumbo (appendix) huakisi umbo la sehemu ya mwili inayorejelewa ambayo ni kifuko kama kidole ambacho kipo sehemu ya chini ya utumbo mkubwa.
Uakisi wa sauti au mlio.
Uakisi huu hubainika pale ambapo leksia huhusika kudhihirisha mfanano wa kisauti au mlio baina yake na kirejelewa.
Mifano.
Pikipiki mlio, pik… pik… piki
Kuku mlio, ku… ku… ku…ku
Cherehani mlio, cherr…cherr…cherr…cherrr…
Uakisi wa tabia.
Baadhi ya leksia katika lugha huakisi tabia za kirejelewa.
Kwa mfano neno Kifaurongo ambalo limeundwa kutokana na maneno mawili kufa na urongo. Huyu ni mdudu apatikanaye kwenye kokwa la embe ambaye akiguswa hujikunja na kukaa kimya kama kwamba amekufa. Hivyo basi neno kifaurongo huakisi tabia ya mdudu huyo.
Kuradidi
Hii ni mbinu ya kurudia neno au sehemu ya neno ili kuleta maana mpya.
Kwa mfano; kizunguzungu, pilkapilka, pikipiki, polepole.
Uwawilishaji/ Uhamishaji
Mbinu hii inahusu kuhamisha vipashio vya neno ili kuchukua nafasi tofauti katika neno jipya linaloundwa.
Pia uhamishaji maana wa neno la awali hupata maana mpya.
Tazama; Vyaa (kwa maana ya zaa ) tunaunda avya ( kuhamisha sauti).
Kupe (mnyama anayenyonya ngombe damu) linatumika kwa mtu anayewategemea mwingine.
Kifaru (mnyama) linapata maana ya gari la vita
Ugeuzaji
Hapa neno linageuzwa kutoka kikundi kimoja kisarufi na kuingizwa katika kikundi kingine.
Kwa mfano; mchezo - mchezaji
okoa - mwokozi, wokovu
***Tathmini kila mbinu ya uundaji wa maneno kisha baadaye uonyeshe ubora na udhaifu wa kila mojawapo.
Matatizo katika Uundaji wa Maneno
Maneno kubeba uzito kimaana. Tatizo hili linaweza kutatuliwa iwapo maneno yatatumika mara nyingi ili yazoeleke, hasa maneno ya kisayansi na kiteknolojia.
Kuwepo kwa istilahi au maneno mbalimbali kwa neno moja.
nomino, jina, nauni
runinga, televisheni
Kutokuwa na utaratibu maalum. Ukosefu wa ruwaza moja. Kwa mfano katika somo la Biolojia;
Plasmagene - utoroji
Plasmalema - ugoziuwili
Plasmadesta - kiuzichembe
Maneno mengine yanakosa “ukubalifu wa kimataifa”.
Katika sayansi baadhi ya maneno yametungwa lakini inaonekana kwamba yanakosa ukubalifu wa kimataifa na ingekuwa mwafaka zaidi kama yangekopwa na kuswahilishwa moja kwa moja.
Neno Neno lililopendekezwa Neno ambalo lina umataifa
Mirage Mazigazi Miraji
Ukosefu wa kutosanifisha istilahi ni pigo kubwa katika somo la isimu kwa mfano, sauti za /m, n, ng' na ny/ huitwa sauti za nasali /nazali / vingongo au vipua.
Dhana zilizotoholewa hasa katika lugha za Kiafrika ni ngumu kufasiri ikiwa mtu hajui lugha asilia ambamo neno hilo limetoka.
Kutafsiri istilahi katika lugha za kigeni mara nyingine hupotosha dhana msingi iliyokuwa katika ya lugha chasili.
UCHANGANUZI WA SENTENSI
Uchanganuzi wa sentensi hufanywa kwa kuzingatia viwango hivi.
Sentensi
Kishazi
Kirai
Neno
Mofimu
Uchanganuzi huu hufanywa kwa njia mbalimbali;
Njia ya matawi
Jedwali
Mstari/ Mshale
Tazama mifano hii:
Sentensi sahili
Njia ya matawi
Baba analima.
S
KN KT
N T
Baba analima
Baba a- na- lim-a.
Msichana na mvulana wameamka mapema
S
KN KT
N U N T E
Msichana na mvulana wameamka mapema.
M-sichana na m-vulana wa-me-amk-a mapema.
Atasoma
S
KN KT
Ø (W ) T
(Yeye) atasoma
Yeye a-ta- som - a.
Jedwali
Baba analima.
S
KN
KT
N
T
Baba
Analima
Baba
a-na-lim-a
Msichana na mvulana wameamka mapema
S
KN
KT
N
U
N
T
E
Mvulana
na
msichana
wameamka
mapema
m-vulana
na
m-sichana
wa-me-amk-a
Mapema
Atalima
S
KN
KT
Ø (W)
T
(Yeye)
atasoma
(Yeye)
a-ta-som-a
Msitari
Baba analima.
S KN+KT
KN N
N Baba
N Baba
KT T + E
T analima
T a-na-lim-a
Msichana na mvulana wameamka mapema
S KN+KT
KN N+U+N
N msichana
U na
N mvulana
N m-sichana
U na
N m-vulana
KT T + E
T wameamka
E mapema
T wa-me-amk-a
E mapema
Atalima
S KN+KT
KN Ø (W)
Ø (W) (Yeye)
KT T
T atalima.
Ø (W) (Yeye)
T a-ta-lim-a
Sentensi ambatano
Baba analima ilihali mama anapika
Matawi
S
S 1 U S2
KN KT KN KT
N T U N T
Baba analima ilhali mama anapika
Baba a- na- lim-a ilihali mama a-na-pik-a
Njia ya jedwali
S
S1
U
S2
KN
KT
KN
KT
N
T
U
N
T
Baba
Analima
ilhali
mama
Anapika
Baba
a-na-lim-a
ilhali
mama
a-na-pik-a
Njia ya mtari au mshale
S S1 + U + S2
S1 KN+KT
KN N
N Baba
KT T
T analima
N Baba
V a-na-lim-a
U ilhali
S2 KN+KT
KN N
N mama
KT T + E
T anapika
N mama
V a-na-pik-a
Sentensi changamano
Mtoto aliyepotea amepatikana leo.
S
KN KT
N T E
Mtoto aliyepotea jana jioni amepatikana leo.
S
KN
KT
N
S
T
E
Mtoto
aliyepotea jana jioni
amepatikana
Leo
M-toto
a-li-ye-pote-a jana jioni
a-me-pat-ikan-a

KN N + S
KN N
N mtoto
S aliyepotea jana jioni
N m-toto
S a-li-ye-pote-a jana jioni
KT T + E
T a-me-pat-ikan-a
T leo
Dhana za Sarufi miundo virai
Kifundo tamati — Ni aina ya vifundo ambavyo havimiliki vingine au haviongozi vingine.
Kifundo ambacho si tamati - vinaweza kunyambuliwa kwa kutumia sheria za kuandika upya. Vifundo ambavyo si tamati humiliki vingine. Vifundo tamati hujenga mkufu tamati.
Baba analima.
1………………………………….. S
2………………. KN KT
3……………….N T
4……………….Baba analima
5………………Baba a- na- lim-a.
1,2,3 vifundo ambavyo si tamati (Makundi).
4 kifundo tamati (Kategoria za maneno)
5 mkufu tamati (Mofimu).
Jina amilifu - Jina amilifu huonyesha kazi/jukumu la kiambajengo fulani katika kielelezo tungo. Mfano Kiambajengo kinachotekeleza kazi ya;
KN kama vile (baba)
KT kwa mfano (analima)
Jina kategoria huonyesha kategoria ya viambajengo kama vile nomino (N), kitenzi (T).
Sheria huru - Sheria huru hutumiwa kunyambua mkufu wowote ule. Hazifungwi na muktadha.
Kitenzi - elekezi - Kitenzielekezi ni kitenzi ambacho hakijitoshelezi kimawasiliano bila yambwa. paka alishika ……………../nini?). Alishika ni kitenzielekezi.
Kitenzikisoelekezi - Kitenzi ambacho kinajitosheleza kimaana bila yambwa ni kitenzi kisoelekezi. Kwa mfano; paka alikufa jana
(i) paka alishika …………..
(ii) paka alikufa.
Uchamko
Huku ni kule kuzalisha sentensi au viambajengo vingi bila kikomo kutokana na kanuni
KN1 KN2 S
KN2 KN3 S
Udhaifu wa Nadharia ya Sarufi Miundo kwa ujumla
Wanamiundo walichukulia kwamba sentensi zote zinafanana na kutofautiana kwa kiasi fulani.
Walionelea kwamba sentensi hazikuwa na uhusiano mwingine isipokuwa muundo wake.
Hawakuzingatia umbo la ndani na nje na mahusiano yao.
Walishughulikia tu umbo la nje.
Hawakuelezea jinsi ya kuchanganua sentensi zenye utata.
Walishughulikia tu hadhi ya vipashio tofauti.
Hawakuzingatia maana ya sentensi.
Udhaifu wa miundo virai
Huonyesha tu uchanganuzi wa tungo ambazo ni za mtindo mmoja.
Uchanganuzi wa sarufi miundo virai hauonyeshi kwa nini katika karibu lugha zote za ulimwengu KN hujitokeza katika nafasi sawa hivi kwamba, lazima iwe ni S KN + KT.
Uchanganuzi wa sarufi miundo virai hauwezi kueleza na kuchanganua tungo ambazo hazina ruwaza ya moja kwa moja au mfululizo/mfuatano. Kwa mfano
Je, umempata Juma
Lo, mbona hivi
Mtindo wa sarufi miundo virai huruhusu tu uchanganuzi na upanuaji wa kanuni moja baada ya jingine. Kigezo cha iktisadi ambacho ni kigezo cha isimu kinachohitaji uchanganuzi hulenga katika kutumia kanuni/vipashio vichache zaidi kadri iwezekanavyo kinakosa kutumika hapa. Mtindo wa uchanganuzi wa sarufi miundo virai hautumii iktisadi.

0 Comments