Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Chimamanda Ngozi Adechie ndiye mwandishi kijana anayenivutia zaidi



Chimamanda Ngozi Adechie, katika picha ya mwaka 2013: picha kwa msaada wa mtandao.
Mwandishi Huyu wa hadithi fupi pamoja na riwaya amezaliwa mwaka 1977 huko Enungu state Nigeria.
Elimu ya juu ameipata katika vyuo vya Eastern Connecticut State University (BA), John Hopkins University (MA) na Yale University MA. Chimamanda ameanza kuwika pale alipotajwa katika tuzo za MacArthur fellowship (2008)  akiwa na umri wa miaka 31.

Baadhi ya kazi zake alizoziandika ni
-Americanah
-Half of yellow sun
-We should all be feminist
-The thing around your neck
na -Dear IJEWELE, Hizi ni chache miongoni kwa kazi lukuki alizoziandika msanii Huyu.

Aidha kazi zake zinazungumzia maisha halisi ya mwafrika katika bara lake na hata nje ya bara lake, Ufeministi na maswala mengine ya kijamii, kitamaduni, kisiasa na kiuchumi ni miongoni kwa masuala yanayojadiliwa katika kazi zake.


PROFESA JOHN MBELE, anasemaje kuhusu Adechie?
Kwa maneno yake mwenye prof mbele katika mtandao wake aliandika

"Riwaya yake ya kwanza, Purple Hibiscus, niliifundisha hapa chuoni St. Olaf. Inavutia sana kwa dhamira, maudhui, na matumizi ya lugha. Inaongelea maisha ya familia ya profesa wa chuo kikuu cha Nsukka, Nigeria, kwa namna ya kukufanya msomaji ujisikie uko sehemu hiyo. Matukio na migogoro baina ya wahusika imeelezwa kwa uhalisi wa kuvutia.

Mwaka 2006 nilipata bahati ya kumwona Chimamanda Ngozi Adichie, alipofika mjini Minneapolis kwenye tamasha la vitabu. Alikuja kuzindua kitabu chake cha pili, Half of a Yellow Sun. Nilinunua nakala, ambayo aliisaini, na tulipata muda wa kuzungumza kiasi, hata akaniambia kuhusu anavyoendesha blogu. 


Sababu inayofanya avutie katika uandishi wake ni uhalisia katika maandishi yake. hakika ninaweza kukiri kuwa Huyu ndiye mwandishi kijana anayenivutia zaidi. Kazi zake zote zinapatikana zinapatikana katika mtandao kama amazoni hivyo unaweza kupata fursa ya kuzisoma.

E. Mashele.

Post a Comment

0 Comments