Header Ads Widget

Responsive Advertisement

HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI KWA MUJIBU WA IRERI MBAABU



E. Mashele
Profesa Ireri mbaabu ni profesa katika chuo kikuu cha Kenyatta katika Kitabu chake cha "historia ya usanifishaji kiswahili ameeleza kwa kina historia ya lugha ya kiswahili na hapa tutapitia madondoo muhimu.
-kiswahili chanzo chake ni uswahilini - pwani ya kaskazini mwa Kenya, kati ya Lamu na mahali ambapo mto Tana huingia baharini. Kilienea kusini hadi Mombasa, Unguja, Kilwa na  kaskazini kuelekea upende wa Mogadishu Somalia
- Athari za waarabu kwa waswahili zilianza kuenea katika karne ya Tisa na kumi.
-Iwapo kweli neno Swahili ni laasili ya kiarabu, basi wangozi walipewa jina hilo wakati huo.
- Waswahili walivamiwa na kutekwa nyara na waarabu kwa karne nyingi
-Waarabu waliishi na waswahili kwa muda mrefu sana na kwamba baadhi yao waliathiriwa kwa kuoana.
-Ndoa zilikuwa ni za upande mmoja tuu ambapo mwanaume wa kiarabu ndio waliowaoa wanawake wa kiswahili.
-kitamaduni wanawake wa kiarabu walikaa nyumbani mpaka walipoolewa
-ingawa waswahili walijiunga na dini mpya ya kiislamu walihifadhi utamaduni wao na lugha yao ya kiswahili.
-Iliwabidi waarabu kujifunza lugha ya wengi ya kibantu nayo ilikuwa kiswahili.
-Kiswahili kilibakia lugha ya kibantu kama vile, Kikuyu, kiluganda au Kinyamwezi.

-waswahili na waarabu walitawala pwani kwa karne nyingi. Vita baina ya mji na mji kama vile, Mombasa kuvamia malindi, malindi kupigana ma lamu, pate na kila viliyokea tu katika miji ya visiwank na pwani na eneo bara lililokuwa karibu.
-Kufikia karne ya 19 kiswahili kilikuwa lugha Kuu ya waarabu wa afrika mashariki.
-Mawasiliano yaliendelezwa kwa lugha ya kiswahili, iliyoandikwa kwa hati za kiarabu hadi kuanzishwa kwa hati ya kirumi na wanaelimu wa zamani kama vile Dkt Krapf na Askofu Steere

Mapitio
Mbaabu E.(2007) Historia ya Usanifishaji wa Kiswahili. Tuki: Dar es salaam

Post a Comment

0 Comments